Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akishuhudia
mmoja wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akitia saini kumdhamini kwenye
fomu yake ya kugombea Urais wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu ujao kwa tiketi ya
chama hicho, katika ofisi ya CCM wilaya ya Kaskazini ‘B mkoa wa Kaskazini
Unguja Zanzibar jana, ambapo alipata wadhamini zaidi ya 1500 katika mikoa yote mine
ya Unguja. Katikati ni Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wilaya hiyo, Haji Machano Haji. Picha zote na
John Badi
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akilakiwa
na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) wa Mkoa wa Mjini Unguja, baada ya kuwasili kwenye ofisi ya CCM wilaya ya
Aman kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania
urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza
kupata wadhamini zaidi ya 1500 katika mikoa yote minne ya Unguja.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati), akipokea
fomu kutoka kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kati, Ally Yusuf
Salim zilizojazwa na wanachama wa CCM mkoa wa Kusini Unguja jana kwa ajili ya
kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya
chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1500 katika mikoa yote minne
ya Unguja. Kushoto ni Katibu wa CCM Kata ya Jumbi, Christina Athony.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati) akifurahia
jambo pamoja na wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Mjini Unguja, kwenye ofisi ya CCM wilaya ya Aman jana
waliofika kumdhamini ili awanie Urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya
chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1500 katika mikoa yote minne
ya Unguja.
No comments:
Post a Comment