HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 15, 2015

SEMINA YA BENKI YA CRDB YA VIONGOZI NA WATUMISHI WA HALMASHAURI ZA KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti Huduma kwa Wateja Tully Mwambapa akizungumza kwenye semina iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kuhusu huduma za fedha zinazotolewa na benki hiyo kwa serikali. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi na watumishi wa Halmashauri za Mikoa ya Kanda ya Ziwa. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika semina hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraza Konisaga akizungumza wakati wa semina hiyo.
Mkuuwa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo akizungumza katika semina hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Hawa Ghasia akifungua semina ya viongozi wa halmashauri za kanda ya ziwa iliyofanyika jijini Mwanza.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa hotuba yake wakati wa semina ya viongozi wa halmashauri ya za kanda ya ziwa iliyofanyika jijini Mwanza. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Hawa Ghasia akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei mara baada ya kufungua semina ya viongozi wa halmashauri za kanda ya ziwa iliyofanyika jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akipeana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo baada ya kutoa hotuba yake kwenye semina ya viongozi wa halmashauri za kanda ya ziwa iliyofanyika jijini Mwanza.
 Sehemu ya viongozi na watumishi wa Halmashauri za Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakifuatilia mada katika semina hiyo.
 Mkurugenzi wa Idara inayohusika na huduma za fedha kwa Serikali, Philip Alfred akielezea namna Benki ya CRDB ilivyojipanga katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa halmashauri mbalimbali nchini.
Sehemu ya viongozi na watumishi wa Halmashauri za Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakifuatilia mada katika semina hiyo.
Mwalimu wa Ujasiriamali na Uhamasishaji, James Mwang’amba akitoa mada ya uhamasishaji. 

No comments:

Post a Comment

Pages