HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 02, 2015

BENKI YA CRDB YASAIDIA KAMATI YA AMANI YA DINI


Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa  akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi hundi ya Shilingi milioni 12 kwa ajili maandalizi ya Futari iliyoandaliwa na Kamati ya Amani ya Viongozi wa Madhehebu ya Dini. Kulia ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum.  
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum wakionyesha hundi ya shilingi milioni 12 kwa ajili ya maandalizi ya futari iliyoandaliwa na Kamati ya Amani ya viongozi wa Madhehebu ya dini itakayofanyika Ijumaa Julai 3 kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum  akitoa shukrani zake baada ya kupokea hundi ya sh. milioni 12 kutoka benki ya CRDB.
 Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Mbalali, Chibby Chibby akiwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum.
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Mbalali, Chibby Chibby akibadilishana mawazo na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Pages