HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 21, 2015

NHC YATOA MSAADA WA MASHINE ZA MATOFALI, SH. 500,000 KWA VIJANA WALIOACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KIGOGO, DAR

 Vijana waliopata ushauri nasaha wa kuacha kutumia dawa za kulevya, wakishangilia baada ya Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Muungano Saguye (aliyevaa koti) kuwakabidhi msaada wa mashine tatu za kufyatulia matofali pamoja na mtaji wa sh. 500,000 katika hafla iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kigogo, Dar es Salaam jana.  Katikati mstari wa mbele ni Mchungaji wa kanisa hilo, Jackson Haranja ambaye pia ni mlezi wa vijana hao wapatao 40. Kulia mstari wa mbele ni Yahya Charahani ambaye ni Ofisa Mawasiliano wa NHC. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Saguye akimkabidhi mashine hizo Mlezi wa vijana hao, Mchungaji Haranja
 Mchungaji Haranja akitoa shukurani kwa shirika hilo baada ya kupokea msaada huo ambapo aliseama utasaidia sana kuinua hali ya maisha ya vijana hao waliokuwa wameathirika na dawa za kulevya
Saguye akizungumza na vijana hao kuhusu lengo la kuwapatia msaada wa mashine hizo.

No comments:

Post a Comment

Pages