Hatua
ya Robo Fainali ya michuano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame
Cup 2015) inatarajiwa kuanza kesho Jumanne kwa michezo miwili kuchezwa katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo
wa kwanza utakua ni kati ya Mabingwa mara tatu wa michuano hiyo timu ya APR ya
Rwanda itakayotoshuka dimbani saa 7:45 mchana kucheza na vijana wa Kwesi Appiah
timu ya Al Khartoum kutoka nchini Sudan.
Saa
10:15 kamili jioni, Gor Mahia mabingwa wara tano wa michuano ya Kagame
watashuka dimbani kucheza na Malakia kutoka Sudan Kusini, viingilio vya michezo
hiyo ya jumanne cha chini kitakua ni elfu tatu (3,000) na kiingilio cha juu
kitakua ni elfu kumi na tano (15,000).
Robo
fainali zitaendela siku ya jumatano, ambapo michezo miwili itachezwa katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam huku macho na masikio ya wapenzi wa mpira
Afrika Mashariki yakielekezwa kwa mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC.
Kabla
ya mechi hiyo ya wapinzani wa soka nchini Tanzania kuchezwa majira ya saa 10
jioni, mchezo wa kwanza utazikutanisha timu za KCCA ya Uganda dhidi ya Al
Shandy kutoka nchini Sudan.
Viingilio
vya mchezo wa siku ya jumatano, kiingilio cha chini ni shilingi elfu tano
(5,000) na kiingilo cha juu kitanua ni elfu ishirini (20,000).
Katika
hatua hiyo ya robo fainali endapo timu zitacheza kwa dakika 90 na mchezo
kumalizika kwa sare, hatua itakayofuata ni kumpata mshindi kwa matuta (penati).
CECAFA YAIPA ONYO GOR MAHIA
Baraza
la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeiandika
barua ya onyo klabu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya kufuatia kuonyesha vitendo
vya utovu wa nidhamu katika michezo yake miwili ya kwanza.
Katika
barua hiyo ya CECAFA kwenda kwa Gor Mahia, imeutaka uongozi huo kuhakikisha
kocha wake Frank Nutal na kikosi kizima kinafuata taratibu za mashindano na
kanunu zilizopo zinazoongoza michuano hiyo.
Kamati
ya uendeshaji wa michuano hiyo (LOC) iliwasilisha malaliko kwa uongozi wa
CECAFA juu ya tabia ya utovu wa nidhamu iliyoonyeshwa na kocha mkuu wa Gor
Mahia, na kitendco cha kuvunja kitasa cha mlango ili kuingia uwanjani.
ZUNGU AZINDUA AIRTEL RISING
STAR
Mbunge
wa Ilala, Mussa Zungu leo amezindua michuano ya Airtel Rising Star kwa mkoa wa
Dare salaam, ambapo timu kutoka wiliya za Ilala, Temeke na Kinondoni
zinashikriki michuano hiyo.
Akifungua
michuano hiyo, Zungu amewatka vijana kutumia vizuri nafasi hiyo ya michuano ya
Airtel Rising kuonekana, kwani kutawapelekea kupata nafasi ya kucheza katika
timu kubwa na kuweza kuendesha maisha yao kwa kupitia mpira wa miguu.
Michuano
ya Airtel Rising Stars imekua ikifanyika kila mwaka nchini kwa lengo la kusaka
na kuibuka vipaji vya wachezaji wenye umri chini ya miaka 17, ambapo wachezaji
wenye vipaji huchaguliwa na kupelekwa katika vituo vya kufundisha soka na
wengine huchaguliwa katika kikosi cha Taifa cha Vijana (Serengeti U17).
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment