Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva, Januari 18, 2025, amefanya ukaguzi wa mradi wa uchimbaji wa kisima kirefu katika eneo la chanzo cha maji Sinde, Manispaa ya Lindi.
Mradi ambao unatekelezwa na wataalamu wa ndani kwa uwezeshaji wa Ofisi ya Meneja wa RUWASA Wilaya ya Lindi, kwa kushirikiana na Chombo cha Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii cha Kuchele (CBWSO). Kisima hicho, ambacho utekelezaji wake umekamilika, kina ukubwa wa inchi 8 na kimegharimu shilingi milioni 39.
Akitoa taarifa ya mradi huo, Mhandisi William Swila ameeleza kuwa kisima hicho kina urefu wa mita 175 na kinatarajiwa kutoa maji lita 60,000 kwa saa moja, huku kikitarajiwa kuhudumia wananchi wasiopungua 25,000. Amefafanua kuwa kazi zilizotekelezwa ni pamoja na utafiti wa maji ardhini, uchimbaji wa kisima, usafishaji wa kisima pamoja na shughuli nyingine za kitaalamu zinazohusiana na ujenzi wa mradi huo..jpeg)
Aidha, Mhandisi Swila amebainisha kuwa mradi huo utaondoa changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama katika kata tano za Halmashauri ya Mtama. Ameongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika azma ya kumtua mama ndoo kichwani.
Kwa upande wake, Mhe. Mwanziva amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusambaza Magari ya kuchimba visima nchi nzima na Lindi nayo kunufaika na gari gilo.
.jpeg)
DC Lindi amepongeza Wizara ya Maji, RUWASA, CBWSO pamoja na wataalamu wote walioshiriki katika utekelezaji wa mradi huo, huku akisisitiza kuwa Serikali ina dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo yanayogusa moja kwa moja maisha ya wananchi, hususan katika sekta muhimu kama maji.
Ametoa wito kwa wananchi kuitunza na kuilinda miundombinu ya maji ili kuhakikisha inakuwa endelevu na inaendelea kutoa huduma bora, safi na salama kwa muda mrefu..jpeg)
Naye Bi. Ashura Chimbuli, mkazi wa Kijiji cha Navanga na mmoja wa wanufaika wa mradi huo, ameishukuru Serikali kwa juhudi kubwa ilizozifanya katika kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.
“Namshukuru Mhe. Rais Mama Samia kwa kutuletea mradi huu mkubwa wa maji kwa Tarafa ya Sudi, Tunaamini mradi huu mara tu utakapoanza kufanya kazi, utasaidia sana kumtua mama ndoo kichwani, tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali,” amesema Bi. Ashura.
.jpeg)


No comments:
Post a Comment