Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum Lager imetoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya wenyeji Uganda (The Cranes) katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2017 nchini Rwanda uliofanyika uwanja wa Nakivubo.
Stars ambayo imeonekana kabadilika katika mchezo wa leo, ilicheza soka la kuvutia tangu mwanzo mpaka mwisho wa mchezo hali iliyowaduwaza wenyeji Uganda.
Mpaka dakika 45 za mchezo za kipindi cha kwanza zinamalizika, Uganda 0 - 0 Tanzania. Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kufanya mashambulizi mfululizo kupitia kwa washambuliaji wake John bocco na Rashid Mandawa.
Dakika ya 58, John Bocco aliipatia Tanznaia bao la kwanza kwa mkwaju wa penayi kufuatia mlinzi wa Uganda Bakaki Shafik kuunawa mpira wa ndani ya eneo la hatari.
Mara baada ya bao hilo Uganda walifanya mashambulizi mfululizo langoni mwa Stars na kufanikiwa kupata bao la kusawzisha dakika ya 82, kupitia kwa mchezaji Kizito Hezron.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Uganda 1 - 1 Tanzania. Kwa matokeo hayo Uganda wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 4 - 1 na sasa watakutana na Sudan.
Mara baada ya mchezo huo kochaa mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema anashukuru vijana wake wamejitahidi kucheza vizuri, mchezo ulikua mzuri timu ilitengeneza nafasi chache na kuweza kutumia nafasi moja iliyopatikana.
Mkwasa amewaomba watanzania kuendelea kuwapa sapoti, wamekaa na timu kwa muda mfupi wa wiki moja tu lakini katika mchezo wa leo mabadiliko yameonekana, hivyo wanahitaji muda kidogo kuweza kukaa na vijana kwa muda mrefu ili kujenga timu bora.
Stars inatarajiwa kurejea Tanzania siku ya jumatatu mchana kwa usafiri wa shirika la ndege la Rwanda Air.
Taifa Stars: Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Haji Mngwali, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Frank Domayo,/Said Ndemla John Bocco, Rashid Mandawa/Salum Telela, Saimon Msuva/Ramadhan Singano.
The Cranes: James Alitho, Muzamiru Mutyaba, Brian Ochwo, Hassan Waswa, Denis Oola, Faruk Miya, John Shemazi/Robert Sentongo, Bakaki Shafik, Tekkwo Derick/Kizito Hezron/Kalanda Frank.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment