Shirikisho
la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) leo limetoa ratiba ya fainali ya
michezo ya Afrika (All African Games), ambapo Timu ya Taifa ya Tanzania
ya Wanawake (Twiga Stars) imepangwa kundi A pamoja na wenyeji
Congo-Brazaville.
Katika
droo iliyochezwa leo makao makuu ya CAF - Cairo na kupanga makundi ya
fainali hizo za michezo ya Afrika, Tanzania imepangwa kundi A pamoja na
wenyeji Congo - Brazaville, Nigeria na Ivory Coast, huku Kundi B likiwa
na timu za Cameroon, Afrika Kusini, Ghana na Misri.
Kundi
B lenye timu ya Twiga Stars linaonekana kuwa ndio kundi gumu zaidi
kutokana na kuwa timu ya Nigeria, mabingwa mara mbili wa michuano hiyo,
wenyeji Congo -Brazzavile washiriki mara mbili wa fainali hizo na timu
ya Ivory Coast.
Twiga
Stars ilifanikiwa kukata tiketi ya kucheza fainali hizo baada ya
kuiondoa timu ya Taifa ya Zambia ya wanawake (She-Polopolo) kwa jumla ya
mabao 6-5.
Fainali hizo za michezo ya Afrika zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi nchini Congo - Brazzaville Septemba 3 - 18 mwaka huu.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment