MKUU wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akishirikiana na
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Issaya Mngurumi, wametoa siku mbili kwa
wafanyabiashara ndogondogo (Wamachinga), waliovamia eneo la Jangwani kuwa hadi
Jaulai 30 wawe wameondoka.
Kauli hiyo inakuja siku moja baada ya Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kuutaka uongozi wa Manispaa
ya Ilala kusitisha zoezi la ugawaji wa eneo la Jangwani kwa wafanyabiashara
ndogo ndogo (machinga) kwa kuwa eneo hilo si salama.
Akizungumza na wandishi jijini Dar es Salaam, Mushi,
alisema kuwa Manispa hiyo haijagawa eneo hilo kama inavyodaiwa wafanyabiashara
hao.
Alisema, wamefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa eneo
hilo limevamiwa na watu ambao hawakuwa lengo la manispaa hiyo kwani
waliyotakiwa kwenda pale walikuwa ni wamachinga wanaotandika biashara zao chini
katika eneo la Kariakoo.
Mushi, alisema baada ya siku mbili hizo kupita manispaa
hiyo itatumia nguvu kuwaondoa katika eneo hilo tena bila kujali gharama
walizoingia katika ujenzi huo.
“Ni vema wakazitumia siku hizi mbili kuboa mabanda yao ili
kuepuka hasara ambayo inaweza kujitokeza baada ya muda uliyotolewa kupita,”alisema
Mushi.
Mushi, ambaye baadhi ya wafanyabishara hao walidai kuwa
alikuwa ni mmoja wa viongozi alitoa agizo la wao kwenda katika eneo hilo,
alipinga vikali kuhusika katika mpango huo.
“Mimi sina maeneo mwenye maeneo ni Halmashauri ya Ilala kwa
hiyo siana uwezo wa kugawa maeneo kama wanavyodai,”alisema Mushi.
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mngurumi, aliwataka
wafanyabiashara hao kutekeleza agizo haraka kabla muda haujapita kinyume chake
atapeleka greda kwa ajili ya kuvunja mabanda yote.
“Kumetokea upotoshaji kwani wakati wanawapeleka
wafanyabiashara hao wa Kariakoo tuliwaeleza wazi kuwa hawana ruhusa ya kujenga
mabanda bali walikubaliana kuwa wataendesha biashara zao kwa kuzitandika
chini,”alisema Mngurumi.
Mwanasheria wa
Baraza hilo, Manchare Suguta, alisema, wakiwa wasimamizi wa mazingira
wamelazimika kuwaandikia uongozi wa manispa hiyo barua Julai 24 mwaka huu
wakiwataka kusitisha uamuzi wao haraka.
Baada ya mkutano huo wa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi,
Tanzania Daima, ili watafuta viongozi wa wamachinga kwa ajili ya kuzungumzia
agizo hilo, hata hivyo walikataa kusema lolote kwa madai kuwa walilkuwa kwenye
mkutano wa kujadili kauli hiyo.
No comments:
Post a Comment