HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 23, 2015

Wanging’ombe; Sasa hatumuelewi Nyimbo, tumemchoka

Na Bryceson Mathias, Njombe

Thomas Nyimbo
WAKATI Watia Nia 12 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakijitokeza kutaka Jimbo la Wanging’ombe akiwemo aliyekuwa Mlezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Njombe, Iringa na Mbeya, Thomas Nyimbo, Wananchi wa Wanging’ombe wamemnanga wakisema, hawamuelewi na wamemchoka.

Wakizungumza na Mtandao huu kwa Sharti la kutotajwa Majina yao, Wananchi hao ambao ni CCM na Vyama vya Upinzani wamedai kuwa, kwa sasa hawamuelewi kabisa Nyimbo, na wamemchoka kutokana na tabia yake ya kuhamahama Vyama na kutafsirika kuwa Mamluki.

Waliotia Nia ya Ubunge kwa tiketi ya CCM ambao ni Wazawa katika Jimbo hilo ni pamoja na, Gerson Lwenge, Thomas Nyimbo, Yono Kevela, Kenned Mpumilwa, Malumbo Mangula, Abraham Chaula, Richard Magenge, Petro Dudange, Hoseana Lunogelo, Nobchard Msigwa, Eston Ngilangwa na Abel Badi.
Nyimbo huyo huyo alipokihama CCM alijigamba na kukinanga kuwa, kinajikaanga kwa mafuta yake chenyewe kutokana na kuachia rushwa kwenye chaguzi zake za ndani kuwa ndio kigezo muhimu cha kuwapata viongozi wake, lakini huyohuyo anakula Matapishi yake akitaka uongozi wake.

Akiachana na Chadema alisema, “Nimeachana na Chadema baada ya kubaini kuwa siasa za vyama havina tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla na ni wakati huu sasa wa kuachana na dhana ya vyama vya siasa vituandalie sera, na tunahitaji sasa itungwe sera ya kitaifa ambayo mgombea inabidi atueleze tukimchagua ataitekeleza vipi” alisema Nyimbo.

Nyimbo ambaye amewahi kuwa mbunge wa Chama cha Mapinduzi CCM) kwa miaka 10 katika Jimbo la Njombe Magharibi kabla ya kukimbilia Chadema 2010, alidai atabaki mwanasiasa huru asiye Cama, lakini leo tena anaibukia CCM, hivyo wananchi wanasema, wamemchoka asitegemea Kitu.

“Hawa Mashushu huwa hawaachi Kazi zao ila kuwayumbisha Wananchi, Kumbukeni 1992 alipoitosa CCM, alikuja akitulaghai na Chama cha PONA alichoanzisha kabla ya kujiunga na Chadema, na leo huyo huyo amekiacha Chadema amerejea CCM, ana agenda ya Siri huyo”alisema mmoja wao ambaye ni Mwanachama wa CCM na Mtia Nia anayepambana naye, huku akitaka asitajwe.

No comments:

Post a Comment

Pages