HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 06, 2015

MGOMBEA CCM akataa Kura 20 za Nyongeza; Mmoja atimkia Chadema

Na Bryceson Mathias, Mkonze

MGOMBEA Udiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) , Agustino Mwimbe, ambaye ni mmoja kati ya Wagombea 10 waliogombea Kata ya Mkonzi, amekataa Kura 20 za Mizengwe, alizoongezewa na Wasimamizi wa Uchaguzi, akidai aachiwe Kura zake Mbili (2) alizopigiwa na Wapiga Kura kwenye Uchaguzi.

Katika Mtaa wa Mji Mpya ‘A’ mgombea huyo alipata kura mbili (2), alithibitisha kukataa Kura 20 alizoongezewa na kuwa 22, akidai hizo ni za Rushwa hawezi kuzikubali, na hivyo anawatuhumu Wasimamizi kubaliana kufanya Mchezo Mchafu.
Wasimamizi wanaotuhumiwa kufanya uchafu huo ni Msimamizi wa Kituo, Emmy Mabwai, na aliyefanya Majumuisho ya Matokeo ya Kura zote za Mawakala toka kwenye Vituo, Hilda Msahala, huku Wagombea wakilalamikia, Ada ya Sh.Laki 210,000/-za Mchakato huo kwa Udiwani.

Mwimbe alisema, katika Kituo cha Mji Mpya, Wakala wake ambaye ni Mwanaye, Jeni Agustino Mwimbe, alisema Baba yake alipata Kura mbili (2), lakini wakashangaa katika Majumuisho aliyosoma Msimamizi wa Uchaguzi Hilda kwa Mkurugenzi, alionekana ana Kura 22 badala ya mbili (2).

Mwimbe alidai, pia Wagombea wenzake Wawili, David Bochela, aliyepata Kura 13 waliyeshindana nae, ambaye awali aliongezewa Kura 40 na akawa na Kura 53, ambapo, Adamu Ally, kwa upande wake naye aliongezewa 40.kunyume na Kura alizopata awali.

Msimamizi wa Uchaguzi huo Mabwai, alipotakiwa aelezee ukweli uko wapi kutokana na Malalamiko hayo, Mabwai aliruka Kimanga akisema, alikanusha akisema, yeye hakuwaongezea Kura, bali hizo ndiyo Idadi ya Kura alizopewa na Mawakala, na amewataka wajieleze kwa Maandishi.

Katika Sakata hilo, Edward Mpari (CCM), aliyekuwa Mgombea wa Udiwani katika Kata hiyo na kufanyiwa Mizengwe ya watu wengine kuongezewa Kura, amesusia Uchaguzi huo na kukihama CCM na Kutimkia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), ambako tayari alipokelewa na kuchukua Fomu ya Kugombea Udiwani kwaa tiketi hiyo.

“Ni kweli Nimekihama CCM na kujiunga na Chadema, baada ya kuona hakuna haki ndani ya Chama hicho, isipokuwa kimekithiti Rushwa na Ufisadi mkubwa hata kwenye mambo ya Kawaida tu, Je, kama mambo madogo ni hivyo, katika mambo makubwa itakuwaje?”.alisema Mpari

No comments:

Post a Comment

Pages