Na Bryceson Mathias, Morogoro
Ofisi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Morogoro Mjini, zimevamiwa na Viongozi wake kukimbia, baada
ya kusikika Taarifa za kukatwa kwa Majina ya Washindi wa Kura za Maoni ya Uchaguzi
wa Udiwani Kata za Morogoro, wakipinga Washindi wao kukatwa.
Dosari hiyo inayopelekea kukigawa Chadema
na kukiingiza kwenye Mgogoro, imepingwa na Wanachama walioapa Watahakikisha
wanakikomboa Chama kutoka kwenye Makucha ya baadhi ya Viongozi Mamluki,
wanaodaiwa kutumiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kukihujumu Chadema kwa Goli la
Mkono.
Akizungumza na Mtandao huu, Kiongozi
wa Kanda, Idd Kizota, ambaye muda wote alipoulizwa juu ya Mgogoro huo alikuwa
Mkali kama Pilipili alisema, Mtu yeyote ambaye anaona ameonewa, akate Rufaa
ngazi ya juu, lakini asikusanye watu na kufanya fujo.
Alipoulizwa kwa nini washindi wa
Uchaguzi wamekatwa alidai, Kuna sababu mbalimbali ambazo hakutaja, na
alipoambiwa kuwa Uongozi akiwemo yeye wanatuhumiwa kutumiwa na Chama cha
Mapinduzi(CCM) waweke watu dhaifu kukiharibu Chadema ili kuandaa ‘Goli la Mkono’,
alidai huo ni upuuzi.
“Kama Mtu anadhani ameonewa, anatakiwa kukata
rufaa kwenye Vikao vya Juu. Wengi wawanaolalamika ni Wazuri kwenye Makaratasi, lakini
wakienda kwa Wananchi wanashindwa……, ambapo alipoulizwa mbona wameshinda
alikuwa Mkali na Kufoka, ‘Ujinga Sitaki hata angekuwa nani!”.alisema Kizota.
Wanachama wa Chadema waliohojiwa kwa
nyakati tofauti wakitaka wasitajwe walisema, Chadema Taifa wanatakiwa
kuuangalia upya Uongozi wa Chadema Kanda ya Kati na ule wa Morogoro na Wilaya
ya Mvomero, ili iwekwe ‘Task Force’ kuelekea Uchaguzi Mkuu, kwa sababu hawana
dhamira Njema na Chadema.
Kata zinazolalamikia Ushindi wa Matokeo
ya Kura ya Maoni ya Udiwani na Washindi wao kukatwa ni pamoja na Kihonda Magorofani,
Kirakala, Mazimbu, K/Ndege, Doma, Lukobe (Waliogomea Uchaguzi mpya), Uwanja wa Taifa,
Chamwino ambao inadaiwa Wanalalamikia amewekwa Mgombea toka CCM asiyejua kusoma
na kuandika ili tu, CCM ishinde kwa Urahisi.
Awali kilienezwa taarifa za Kwamba, Mgombea
wa Ubunge jimbo la Mvomero, Matokeo Warden Mang’eta, amekatwa, ambapo Wana
Chadema wa Jimbo hilo walitaka kuanza kutaka kufunga safari kuelekea Dumila
Ofisi ya Wilaya na Kindumbwendubwe Chalia, lakini Kizota alikanusha kuwa
Mgombea huo amekatwa, jambo ambalo Kadi za Chadema zilisalimika Kukuchomwa.
No comments:
Post a Comment