HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 16, 2015

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI WAWATAKA WAAJIRI KUWAKILISHA MICHANGO YAO KWA WAKATI

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Masha Mshomba akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu adhabu zitakazotolewa kwa waajiri wa sekta ya Umma na binafsi pindi watakapochelewesha michango yao. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Uchambuzi Sera SSRA, Angar Mushi. (Picha na Francis Dande)


Na Mwandishi Wetu 

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umewahimiza waajiri wa sekta ya Umma na binafsi kuwasilisha michango  ya wafanyakazi kwa wakati kupitia akaunti za mfuko huo, watakaochelewesha watapewa adhabu kwa mujibu wa sharia ya mwaka 2008 ya mfuko huo.


Akizungumza na waandishi  wahabari jijini  Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia, Masha Mshomba, alisema uchangiaji ulianza Julai mosi mwaka huu kama ilivyoelekezwa katika Tangazo la Serikali Na 169 la Mei,2015., baada ya yeye kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu na  Bodi  ya Wathamini.

“Vifungu hivyo vya sheria vitakavyotumika kuwabana waajiri watakaochelewesha kuwasilisha michango hiyo ni cha 75 (2), (3)  na (4) vya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, Na 20 ya mwaka 2008,alisema Mshomba.


Mshomba alisema katika uchangiaji huo michango ya mwezi wa saba inatakiwa kupelekwa mwezi wa nane na ya mwezi wa nane inatakiwa kupelekwa mwezi wa tisa  katika benki ya NMB (akaunti Na 20110016403,tawi la Bank House), CRDB(Akaunti Na 0150237547300, tawi  la Holland House) au njia nyingine inayokubalika na kinyume cha hapo mwajiri atapewa athabu.

Alisema  lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo ni kutokana na  Serikali kukabilina  na matatizo ya ulipaji wa fidia kwa Wafanyakazi katika Mfumo wa utoaji fidia uliokuwepo awali.

“Matatizo hayo ni pamoja na kiwango kidogo cha malipo ya fidia kiwango kisichozidi shilingi 108,000 kwa ulemavu wa kudumu na shilingi  83,000 kwa wategemezi endapo kifo kitatokea  kwa mfanyakazi husika,uchache wa mafao na urasimu kwa baadhi ya waajiri katika utoaji wa fidia.”alisema Mshomba.

 Mshomba, alisema kwa mujibu wa kifungu cha 2  cha  Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi,Na 20/2008, Mfuko huu unawahusu Waajiri na Wafanyakazi wote katika Sekta ya Umma na sekta binafsi ,Tanzania Bara.

Aliongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2015 hadi 2016 viwango vya uchangiaji kwa kila mwezi ni asilimia moja ya mapato ya Wafanyakazi kwa Waajiri  wa Sekta binafsi na asilimia  0.5 ya mapato kwa  Wafanyakazi kwa Waajiri wa Sekta ya Umma, ambapo michango hiyo ni gharama ua Mwajiri na haipaswi kukatwa kwenye mapato ya Mfanyakazi.

 Mshomba alisema mafao yatakayotolewa na Mfuko huu ni huduma ya matibabu, malipo ya ulemavu wa mudana ulemavu wa kudumu, kwa anaye mhudumia mgonjwa, huduma za ukarabati na ushauri nasaha,gharama za mazishi na malipo  kwa wategemezi wa marehemu.

Naye kaimu Mkurugenzi Hifadhi ya Jamii Wizara ya Kazi na Ajira, Daudi Kaali, alisema mfuko huo unakabiliwa nsa changamoto ya uelewa wa sheria mpya waajiri na wafanyakazi bado hawajajua wajibu wao.

No comments:

Post a Comment

Pages