| Gari la Mgombea Ubunge jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi Sugu likiwa kituo cha Polisi kati jijini Mbeya mara baada ya kushambuliwa kwa mawe. Picha Kenneth Ngelesi Mbeya. |
| Sugu akiwa kituo cha Polisi na wafuasi wake. |
Na Emanuel
Kahema, Mbeya
MGOMBEA
ubunge kupitia chadema jimbo la Mbeya
mjini, Joseph Mbilinyi leo amejikuta
katika wakati mgumu baada ya msafara wake kushambuliwa na watu wasiofahamika na watu wawili wamejeruhiwa akiwemo dereva aliyekuwa akimuendesha mgombea huyo.
Tukio hilo
la kushambuliwa kwa msafara huo, limetokea majira ya saa 11 za jioni katika
eneo la barabarani lililopo katika Kata
ya Ghana mtaa wa Mbata jijini hapa ambapo inasemekana mgombea huyo alikuwa katika harakati za kampeni kuomba kura kwa
wananchi wa Iziwa ambapo mgombea huyo
alikuwa ndani ya gari yake yenye namba za usajili T161 CPP Toyota Land Cruser VX .
Kutokana na
hali hiyo mgombea huyo wa ubunge mbeya
mjini kwa tiketi ya Chadema alilazimika kukatisha zoezi lake la kuongea na
wakazi wa Kata ya Iziwa iliyopo Jijini Mbeya kwa muda, kutokana na kulazimika
kuripoti katika kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa maelezo.
Mgombea huyo
ilimlazimu kufika kituoni na kuchukuliwa maelezo na baada ya hapo aliruhusiwa
kuendelea na shughuli zake za kisiasa lakini gari yake yenye namba za usajili
T161 CPP aliyokuwa akiitumia katika kampeni zake ikibaki polisi.
Hata hivyo,
mgombea huyo alipomaliza kutoa maelezo
katika kituo cha polisi cha kati cha Wilaya ya Mbeya, aligoma kuzungumza
na vyombo vya habari ambavyo vilikuwa kwenye eneo la tukio na kuwataka wafike
katika mkutano kwani ndipo atakapotolea ufafanuzi wa suala hilo hilo.




No comments:
Post a Comment