Uendondo Nkone (katika) akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa mkutano na waandashi wa habari kuhusu kuadhimishi miaka 10 tangu aanze huduma ya uimbaji.
MWIMBAJI
mahiri wa nyimbo za injili nchini Upendo Nkone, kesho anatarajiwa kuadhinisha
miaka 10 tangu aanze huduma hiyo ya uimbaji sambamba na uzinduzi wa albamu yake
ya tano iitwayo ‘Omba Yesu Anasikia’ yenye jumla ya nyimbo.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam juzi, Nkone alisema mbali ya tukio hilo la kesho kubeba uzinduzi wa albamu mpya
na maadhimisho ya miaka yake 10 katika huduma hiyo, pia kwake ni kumshukuru
Mungu kujamlia uzima na afaya.
Alisema
kudumu kwa miaka yote hiyo katika huduma hiyo yenye vikwazo na hila za kila
aina, ni jambo la kumshuruku Mungu ikiwemo kumvusha salama katika matatizo ya
kiafya aliyopata mwaka jana hadi kufanyia upasuaji mkubwa.
“Upendo
wa Mungu ni mkubwa mno kwangu. Kufanya huduma hii ya uimbaji kwa miaka yote hii
10, sio kitu kidogo. Lakini pia kupitia tukio hili la Jumapili (kesho),
nitalitumia kurejesha sifa na utukufu kwa Mungu kunivusha salama katika upasuaji
ambao hata madaktari walikiri ulikuwa mgumu,” alisema.
Kuhusu
uzinduzi huo utakaofanyika katika ukumbi wa Kanisa la TAG-Upanga lililopo chini
ya Askofu Mwasongole, Upendo alisema maandalizi yamekwenda vizuri na
atasindikizwa na waimbaji wengi mahiri katika tukio hilo muhimu kwake.
Anawataja
baadhi ya waimbaji watakaomshindikiza, ni Bonny Mwaitege, Masanja Mkandamizaji,
Messi Chengula, Jesca Boniface Magupa ‘BM’, Bahati Bukuku na wengineo kibao na
kutoa wito kwa wapendwa na wapenzi wa muziki wa injili kujitokeza kwa wingi.
Upendo
alisema tukio hilo litakaloanza majira ya saa nane mchana, kiingilio cha juu kitakuwa
shilingi 5,000 kwa wakubwa na watoto ni shilingi 2000 na kusema kila
atakayefika ukumbini, hatajutia muda wake.
Akizungumzia
mafanikio ya huduma yake, Upendo amemshukuru Mkurugenzi wa Msama Promotions ya
jijini Dar es Salaam, Alex Msama kwa saopoti kwani kupitia matamasha yake ya
Pasaka na Krismasi, yamempa nafasi ya kujulikana na kukua zaidi kihuduma.




No comments:
Post a Comment