MGOMBEA urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema kutokana na kukubalika kwake katika mikoa yote aliyokwenda kufanya mikutano ya kampeni, ana uhakika wa kupata ushindi wa tsunami katika uchaguzi wa mwaka huu.
Amesema katika mikoa yote aliyokwenda kufanya kampeni, wananchi wamemkubali na kumuhakikishia kumpigia kura nyingi ili aweze kuwa Rais wa awamu ya tano ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG - GEITA.
Umti mkubwa wa watu ukifuatilia mkutano wa Magufuli.
Umati.
Tunafuatilia mkutano.

Magufuli akihutubia.
Aidha, Dk. Magufuli alisema uamuzi wake wa kufanya kampeni kwa kutumia barabara umelenga kufika katika maeneo mengi nchini na pia kushuhudia kero zinazowakabili wananchi ili aweze kuzitafutia ufumbuzi.
Aliwaahidi wananchi wa Bushosa kuwa atakapoapishwa na kuwa rais wa Tanzania, atatoa kipaumbele kwa ujenzi wa barabara ya Kamanga hadi Sengerema kwa kiwango cha lami.
Hata hivyo, aliwataka wavuvi katika jimbo hilo na mkoa wa Geita, kujiepusha na uvuvi wa kutumia sumu aina ya thiodan kwa vile unasababisha kutoweka kwa samaki kwenye Ziwa Victoria.








No comments:
Post a Comment