Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Mhandisi Suleiman Suleiman (kulia), ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
mahafali ya 46 ya kidato cha nne Shule ya Sekondari Pugu Dar es Salaam, akipata
maelezo kutoka kwa mwanachama wa Klabu ya Mazingira ya Roots and Shoots wa
shule hiyo jinsi wanavyotumia vipaji vyao kuhihadhi mazingira kwa kutengeneza
kadi za mialiko zisizochafua mazingira, juzi. Wa pili kulia ni Mkuu wa shule
hiyo, Jovinus Mutabuzi. (Na Mpiga Picha Wetu)
Kiongozi
wa Skauti katika Shule ya Sekondari ya Pugu, Dar es Salaam akimvisha skafu, Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S.
Suleiman aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 46 ya kidato cha nne katika
shule hiyo alipowasili ukumbini kuwatunuku vyeti, wahitimu. Kushoto ni
Mkuu wa shule hiyo, Jovinus Mutabuzi.




No comments:
Post a Comment