Timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro Premium Lager, inatarajiwa kusafiri na ndege ya binafsi ya
kukodi ya shirika la Fastjet kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo
wa marudiano utakaochezwa Novemba 17 mjini Algiers.
Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la Fasjet kwa ukanda wa Afrika
Mashariki, Jimmy Kibati amesema kampuni yao imefikia makubaliano na TFF
ya kuwa msafirishaji rasmi wa timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo huo wa
kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi 2018 dhidi ya
Algeria.
Jimmy amesema katika safari hiyo, Fastjet itatoa ndege yenye uwezo wa
kubeba abiria 156 walioketi, sambamba na wafanyakazi wa ndenge, ambapo
wao wametoa punguzo la asilimia 35 katika gharama nzima ya safari ya
kuelekea Algeria.
Aidha Jimmy ameongeza kuwa safari hiyo itakua ni ya masaa 7 ambapo
ndege ikitoka Dar es salaam itatua Djamena – Chad kuongeza mafuta kabla
ya kuendelea tena na safari mpaka nchini Algeria.
Naye katibu wa kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda aliwashukuru
Fastjet kwa kukubali kuwa wasafirishaji rasmi wa TaifA Stars kwa mechi
dhidi ya Algeria, huku akisema gharama za safari za mtu mmoja kusafiri
ni dolla 800 kwenda na kurudi.
Teddy amewaomba watanzania, wapenzi, washabiki wa mpira wa miguu
wanaotaka kusafiri kufika ofisi za TFF zilizopo Karume kwa ajili ya
kujiandiksha na kuelekea taratibu nzima za safari.
No comments:
Post a Comment