MBUNGE mteule wa Muleba Kaskazini (CCM) na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Mwijage akisalimiana na Godson Kaligo Mjumbe wa tawi la CCM Empress Social lililopo mtaa wa Samora maarufu kwa Musa Shoeshine alipowatembelea wakati wa sherehe yao ya kusherehekea ushindi wa Rais Mteule Dr. John Pombe Magufuli mara baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu nchini kote, Wana CCM hao wamesherehekea kwa muziki na kupata supu ya mbuzi na nyama choma huku wakiwakaribisha wananchi mbalimbali bila kujali itikadi zao kwani Dr John Pombe Magufuli ni Rais wa Watazania wote.(PICHA NA RASHID SHOTI-DAR ES SALAAM)
MBUNGE mteule wa Muleba Kasikazini (CCM) na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Mwijage akibadilishana mawazo na Godson Kaligo na wana CCM wa tawi hilo.
Katibu wa Tawi hilo Musa Mtulia ambaye pia ni Shoeshine Maarufu mtaa wa Samora akiendelea na kazi yake huku wana CCM wengine na wadau wengine wakiendelea na sherehe hiyo kwa kupata supu.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa tawi hilo Hassan Mneo. Mjumbe Godson Kaligo pamja na wadau wengine wakipata supu kutoka kulia ni Bw. Haogwa na Mzee Mnonji shabiki maarufu wa timu ya Simba.
Mwana CCM Richard Wambura aliyesimama nyuma naye alijumuika na wana CCM wenzake wakati alipowatembelea tawini hapo
Hapa ni mwendo wa kutafuna mbuzi tu.
Mwenyekiti Hassan Mneo kushoto na we nzake wakipata supu na kahawa katika wtawi hilo.
Katibu wa tawi Musa Mtulia akifurahi na wadau mbalimbali waliofika katika tawi hilo wakati wa sherehe hiyo.
No comments:
Post a Comment