Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchangishaji wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust, Daniel Mwasandube
akifafanua jambo wakati wa hafla ya kutiliana sahihi makubaliano ya kuboresha
Shule za Msingi na Utoaji wa Madawati kati ya Benki M na taasisi hiyo. (Picha
na Francis Dande)
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki M, Jacqueline Woiso (wa pili kulia) akibadilishana hati na Mjumbe
wa Bodi ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust, Balozi Bertha Semi-Somi wakati wa
kusaini ushirikiano wa kuboresha mazingira ya Elimu kwa Shule za Msingi na
Utoaji wa Madawati. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchangishaji, Daniel
Mwasandube na Mkurugezni Mtendaji wa taasisi hiyo, Zena Tenga.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki M,
Jacqueline Woiso (wa pili kulia) akibadilishana hati na Mjumbe wa Bodi ya
Taasisi ya Hassan Maajar Trust, Balozi Bertha Semi-Somi wakati wa kusaini ushirikiano
wa kuboresha mazingira ya Elimu kwa Shule za Msingi na Utoaji wa Madawati.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchangishaji, Daniel Mwasandube na
Mkurugezni Mtendaji wa taasisi hiyo, Zena Tenga.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki M, Jacqueline Woiso (wa pili kulia) akibadilishana hati na Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust, Balozi Bertha Somi baada ya kusaini ushirikiano wa kuboresha mazingira ya Elimu kwa Shule za Msingi na Utoaji wa Madawati. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchangishaji, Daniel Mwasandube.
NA GLORY CHACKY
Taasisi ya Hassan Maajar Trust inakusudia kukusanya shilingi milioni 300 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 1,764 kwa ajili ya Shule ya Msingi Majimatitu Mbagala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa kusaini mkataba wa ushirikiano na Benki M Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust, Balozi Bertha Semi-Somi alisema kuwa taasisi hiyo imesaini mkataba utakaowezesha kuboresha mazingira ya shule za msingi hapa nchini pamoja na utoaji wa madawati.
Taasisi ya Hassan Maajar Trust imeweza kusaidia madawati 7,000 katika Shule za Msingi hapa nchini na kuweza kupunguza tatizo la upungufu wa madawati katika baadhi ya shule zilizokuwa zikikabiliwa na uhaba mkubwa wa madawati.
“Zaidi ya wanafunzi 21,000 kutoka mikoa tofauti hapa nchini waliokuwa wakikaa sakafuni, wamefikiwa na mpango huo na ukikamilika unategemea kuongeza mahudhurio ya wanafunzi mashuleni na hatimaye kukuza na kuboresha kiwango cha elimu nchini".
“Kuwezesha wanafunzi zaidi ya 21,000 kukaa kwenye madawati ni mafanikio ambayo tunapaswa kijivunia, hilo ni moja ya mambo ambayo yametuvutia kuungana tena na taasisi ya Hassan Maajar mwaka huu, sote tunaelewa changamoto zinazokabili sekta ya elimu hivyo ni jukumu letu sote kushirikiana na serikali katika jitihada zake kuikabili changamoto hii”alisema.
Alisema ushirikiano wanaoupata kutoka kwa benki hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 2011, umechangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha miradi yao.
"Tunawashukuru sana wafadhili wetu wote, hususani mshirika wetu Mkuu Benki M”alisema Balozi Semi-Somi" Pia kauli mbiu ya matembezi hayo ni “Walk for a Desk” yatafanyika Novemba 28, yataanzia na kuishia katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Barabara ya Toure Oysterbay.
Hata hivyo Taasisi ya Hassan Maajar mpaka sasa imeweza kutoa madawati zaidi 7,000 ambayo yamepelekwa katika mikoa tofauti hapa nchini ili kupunguza tatizo la wanafunzi 21,000 waliokuwa wakikaa sakafuni na kuongeza mahudhurio ya wanafunzi mashuleni.
No comments:
Post a Comment