HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 23, 2015

CHADEMA WAFUNGUA KESI MAHAKAMANI KUOMBA TAFSIRI YA KISHERIA KUAGWA KWA MWILI WA MAWAZO, LOWASSA AWAJULIA HALI MANUSURU WA MACHIMBO YA NYANGARATA

 Mwanasheria wa Chadema, John Mallya akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, baada ya kufungua kesi mahakamani hapo kuomba tafsiri ya kisheria iwapo aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, marehemu Alphonce Mawazo hastahili kuagwa kwa heshima kama wanavyoagwa Watanzania wengine. (Picha na Sitta Tumma)
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, muda mfupi baada ya kufungua kesi ya kikatiba mahakamani hapo jana, kuomba tafsiri ya kisheria iwapo aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, marehemu Alphonce Mawazo hastahili kuagwa kwa heshima kama wanavyoagwa Watanzania wengine (Picha na Sitta Tumma)
  Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe (katikati mbele) akiwa na viongozi wenzake wa chama hicho wakati wakitoka kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza jana. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalim. (Picha na Charles Mseti)
 Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe (katikati mbele) akiwa na viongozi wenzake wa chama hicho wakati wakitoka kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalim. (Picha na Charles Mseti)
 Askari Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa wameimarisha ulinzi eneo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, wakati wa kufunguliwa kesi ya kuhusu mazishi ya Mawazo. (Picha na Charles Mseti)

Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe (wa tatu kulia waliokaa) na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho taifa Zanzibar, Said Issa Mohamed (wa kwanza kushoto waliokaa) akiwa na viongozi na wafuasi wa chama hicho katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza kwa ajili ya kusikiliza kesi kuhusu kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, marehemu Alphonce Mawazo. (Picha na Sitta Tumma)

 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akimsalimia na kumpa pole mmoja wa wachimbaji wadogo walionusurika kufa kwenye machimbo ya Nyangarata yaliyopo wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, Joseph Burure Robi (44), alipozulu Hospitali ya Wilaya ya Kahama mkoani humo kuwapa pole. Robi alipozinduka hospitalini alihoji iwapo Lowassa ameshinda urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu. (Picha na Sitta Tumma).
 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwasalimia wananchi waliofurika katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga alipokwenda kuwapa pole waathirika wa machimbo ya Nyangarata.
 Wananchi wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wakisukuma gari jana alilokuwa amepanda Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alipokuwa akitoka Hospitali ya Wilaya ya Kahama kuwapa pole waathirika wa machimbo ya Nyangarata walionusurika kifo ambapo wamelazwa hospitalini hapo.

No comments:

Post a Comment

Pages