HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 23, 2015

UTT-PID yashiriki mkutano wa mwaka wa Wanahisa wa UTT-AMIS jijini Dar es Salaam

1 (1)
Maafisa masoko wa UTT-PID, Laurence Nzuki (kushoto) na Martin Mchanjila (katikati) wakitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliotembelea kwenye banda hilo la UTT-PID wakati wa mkutano huo wa mwaka wa Wanahisa wa UTT-AMIS uliofanyika mwishoni mwa wiki, Novemba 21-22.2015, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

Na Andrew Chale, Modewjiblog

Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID) inafanya miradi mbalimbali ikiwemo huduma za uuzwaji wa viwanja katika maeneo tofauti nchini ikiwemo vile vya mradi wa katika miji ya Chalinze na Mapinga Bagamoyo Mkoani Pwani. Pia mradi wa viwanja vya Bunju, Tundwi songani-Kigamboni ambayo ipo Jijini Dar es Salaam. Mingine ni Kingorwila, Madaganya, Mkoani Morogoro. Lindi, Bukoba, Sengerema na kwingine kwingi hapa nchini.

UTT -PID ni miongoni mwa taasisi zinazofanya vizuri na utendaji wa kasi katika utoaji huduma za ushahuri katika maeneo ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.
AsfOxbUQv7XGaXHM7H-QB4HDmtD0NoXc-5OrHiTpRdSO
Picha ya juu na chini Afisa masoko wa UTT-PID, Mary Lugusi akielimisha wananchi juu ya miradi inayoendeshwa na taasisi hiyo kwa wananchi hao waliotembelea banda hilo.
AuISTCaTvV-iYBU-Kfj_MXe9kHuIQPYgU4bZXhQo6OXa
Wananchi wakitembelea banda hilo la UTT-PID..
AmP8BMKF9VkuKPXrXzrxLFNdWA_ZhP3KDMoYW5wunYlG
Mkuu wa Mahusiano ya Umma UTT-PID, Eugenia Simon akiwa pamoja na Mshahuri wa masuala ya uwekezaji wa UTT-Micro finance wakati wa mkutano huo mkuu wa mwaka wa wanahisa wa UTT-AMIS, uliofanyika Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
AnQqTlX1RpGgYJtjKG4oeWsJ-LyltzccztY6XmJx9t4j
Mmoja wa wananchi akipata maelezo kutoka kwa afisa masoko wa UTT-PID, Mary Lugusi.

No comments:

Post a Comment

Pages