Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha la kumshukuru mungu kwa amani na utulivu wakati wa uchaguzi mkuu, Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo. Kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo, Khamis Pembe. (Picha na Francis Dande)
NA
MWANDISHI WETU
KANISA
la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) mkoani Dodoma
limewataka waandaaji wa Tamasha la Kushukuru, Kampuni ya Msama Promotions
kuukumbuka mkoa wa Dodoma katika tamasha hilo linalotarajia kufanyika Desemba 25 katika ukumbi wa
Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam .
Akizungumza hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha Alex Msama
alisema amepokea taarifa hiyo kutoka kwa Mchungaji wa kanisa hilo
mkoani Dodoma ,
Elia Meshack.
Msama
alisema Mchungaji Meshack ameliomba tamasha hilo
ili kufikisha asante yao kwa Mungu baada ya kufanikisha uchaguzi Mkuu wa Tanzania
uliofanyika Oktoba 25 nchini kote.
Aidha
Msama kwa kuwa waliandaa tamasha la kuombea amani uchaguzi Mkuu, hapana budi
kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya kuomba amani katika uchaguzi huo.
“Nimezungumza
na Mchungaji Meshack akinieleza kwamba itakuwa vema Tamasha la Shukrani
nikilifikisha mkoani Dodoma , Kamati yangu
inafanya mikakati ya kuweza kufikisha asante kwa Mungu,” alisema Msama.
No comments:
Post a Comment