HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 19, 2015

Mbunge alitaka Tamasha la Shukrani Mwanza

NA MWANDISHI WETU

MBUNGE  wa Nyamagana Stanslaus Mabula ameiomba Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Kushukuru linalotarajia kufanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, lihamie jijini Mwanza kwa lengo la kufikisha shukrani kwa Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Alex Msama wanayafanyia kazi mapendekezo ya Mabula ili kufanikisha tamasha hilo adhimu lenye nia ya kushukuru Mungu baada ya uchaguzi Mkuu.

Msama alisema tamasha hilo litashirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa Injili ambao watawasilisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani na utulivu.

Msama alisema Kamati yake inajipanga kufikisha ujumbe wa Shukrani kwa Mungu kupitia viongozi wa dini wakiwemo maaskofu na wachungaji wa makanisa mbalimbali hapa nchini.

“Tamasha la Kushukuru Mungu lina mtazamo wa kufikisha asante kwa Mungu baada ya kuendelea kudumisha tunu ya amani ambayo ndio sifa ya Tanzania nje ya mipaka,” alisema Msama.

Aidha, Msama alitoa wito kwa Wadhamini na wafadhili kujitokeza kwa lengo la kusaidia tamasha hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages