Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi. |
Na
EmanuelMadafa, Mbeya
Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba Promis Dank mkazi wa bwawani wilaya ya chunya
alifariki dunia njiani akiwa anapelekwa hospitali baada ya kutumbukia kisimani.
Tukio hilo limetokea Novemba 112 majira
ya saa 12 asubuhi huko kitongoji cha railway, kata ya bwawani, wilaya ya chunya, mkoa wa
mbeya.
Inadaiwa kuwa, mtoto huyo baada ya kutumbukia kwenye kisima hicho
ambacho kilikuwa wazi, aliokolewa akiwa hai lakini alifariki dunia akiwa njiani
kuelekea hospitali teule ya mwambani kwa matibabu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed z. Msangi ametoa wito kwa wazazi na walezi
kuwa makini hasa kwa kuweka uangalizi wa kutosha kwa watoto wadogo ili kuepuka
madhara yanayoweza kuepukika.
Aidha anatoa wito kwa jamii kufunika visima vilivyowazi, kufukia
mashimo yenye maji kwani ni hatari kwa watoto wadogo hasa katika msimu huu wa
mvua za vuli.
(JAMIIMOJABLOG MBEYA )
No comments:
Post a Comment