Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akifafanua jambo kuhusu maandalizi ya tamasha la Krismasi la kumshukuru mungu baada ya kufanikisha uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 25. Kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo, Willy Kapawaga na mwimbaji wa nyimbo za injili, Rose Muhando. (Picha na Francis Dande)
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Rose Muhando moja ya nyimbo zake wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tamasha la Krismasi la kumshukuru mungu baada ya kufanikisha uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 25. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama ambao ni waandaaji wa tamasha hilo.
Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI
mahiri wa muziki wa injili Afrika Mashariki, Rose Muhando, ameanza kujifua kwa
ajili ya kufanya kweli katika Tamasha la Krismas litakalofanyika Desemba 25
katika Ukumbi wa Diambond Jubilee, jijini Dar
es Salaam .
Muhando
mmoja wa waimbaji waliothibitishwa kutumbuiza katika tamasha hilo kwa lengo la kuwaleta pamoja wapenzi na
mashabiki wa muziki wa injili kufurahia tukio la kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu
Kristo, alisema ataimba vibao vyake vya zamani na nyimbo mpya.
“Namshukuru
Mungu kunijalia kipaji na karama ya uimbaji, pia kupata nafasi ya kuwa miongoni
mwa washiriki wa Tamasha la Krismas. Kwa upande wangu ni fursa muhimu kuzidi
kumtukiza Mungu kwa sauti aliyonijalia,” alisema Muhando na kuongeza:
“Nimejiandaa
vizuri kwani wakati wowote mimi nimekuwa nikijiweka hali ya utayari katika
kumtumikia
Mungu
kwa kipaji hiki cha uimbaji.
“Nawalika
wapenzi wa nyimbo za injili na wapendwa wote, waje Diamond Jubilee tufurahie
Krismas na tuseme asante
Mungu kuivusha salama nchi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25,” alisisitiza.
Alisema,
kwa kushirikiana na waimbaji wengine wa ndani na nje ya nchi, watajitahidi kulitendea
haki Tamasha hilo
akiamini ni tumkio la kimataifa hivyo hata maandalizi yake yanapaswa kubeba
uzito huo na siyo vinginevyo.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo ,
Alex Msama, amemtaja Christina Shusho kushiriki Tamasha hilo akiungana na wengine huku waimbaji wengine
wataendelea kujulikana baada ya kukamilika kwa mazungumzo na waratibu.
Shusho,
mwimbaji aliyewahi kutamba na vibao mbalimbali kama Unikumbuke na vinginevyo, yu
miongoni mwa waimbaji waliowajaaliwa kipaji cha kumtumikia Mungu kwa njia hiyo ya
uimbaji kwani ujumbe wa nyimbo zake umekuwa ukiwabariki, kuwajenga wengi
kiimani na kuacha matendo mabaya.
No comments:
Post a Comment