Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF) limeendelea na
kampeni yake ya kuwafata Wakulima mashambani, Katika awamu ya pili ya kampeni
hiyo NSSF imeweka kambi katika Kijiji cha Mtiniko, Mtwara Vijijini ambako
imeweza kutoa elimu kwa wakulima wa Korosho
juu ya Mafao mbalimbali yatolewayo na NSSF.
Katika kampeni hii ijulikanayo kama NSSF kwanza, Shirika
linahamasisha zaidi watu walio kwenye Sekta binafsi waweze jiunga na NSSF ili
kuweza kujipatia Mafao ya matibabu bure kwa Wanachama na familia zao, Mafao ya
kuumia kazini na mikopo kupitia Vikundi vya Ushirika (AMCOS na SACCOS).
Pia NSSF imekuwa ikitumia mikutano hii ili kuweza kupata
mrejesho wa huduma zake kwa wale wakulima ambao tayari wameshajiunga na Mfuko.
NSSF inawasihi wakazi wa Mtwara na vitongoji vyake kutumia
fursa hii ya kujiunga na NSSF.
Wakazi wa Kijiji cha Mtiniko, Mkoani Mtwara wakisubiri kujaza fomu ili wajiunge na NSSF baada
ya kupewa elimu na maafisa wa NSSF kwenye kampeni maalumu ya NSSF Kwanza.
Wakazi wa Kijiji cha Mtiniko kata ya Nanyamba Mtwara Vijijini wakipewa Elimu na Maafisa wa NSSF juu ya faida za kujiunga na NSSF.
Wakulima wa Kijiji cha Mtiniko Mtwara wakijiandikisha ili kujiunga na NSSF baada ya kumalizika kwa mkutano ambao maafisa wa NSSF walikuwa wakitoa elimu juu ya manufaa ya kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii.
Wakazi wa Kijiji cha Mtiniko, Mtwara Vijijini wakiwa
wamekusanyika wakimsikiliza afisa wa NSSF akiwaelezea fursa watakazo zipata kwa
kujiunga na NSSF kwenye mkutano uliofanyika kijijini hapo.
No comments:
Post a Comment