NA KENNETH NGELESI, MBEYA
MAMLAKA ya chakula na dawa TFDA nyanda za juu kusini wanafunzi pamoja na wananchi kuwa makini wanaponuanua vipodozi vinavyouzwa kwa kificho na vile vinavyo tembezwa na wamachinga majumbani kwa kuwa baadhi havina vigezo kwa matumizi ya binadamu kwani vinaweza kusababisha kuharibu uzio wa ngozi na kupenya hadi kwenye damu na kusababisha kansa.
Hatua hiyo imekuja baada ya wafanyabiashara wasio waaminifu kukimbizia sokoni vipodozi hivyo vilivyopigwa marufuku na vingine vinavyotengenezwa na baadhi wajasiliamali katika mazingira ya kificho nayasiyo rasmi bila kupata usajili na kufuata ushauri wa kitaalamu jambo linaloweza kuleta madhara kwa watumiaji.
Akizungumza wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi, Sekondari na Taasisi za elimu ya juu jijini hapa,meneja chakula na dawa nyanda za juu kusini Rodney Harananga katika msako wa kutokomeza vipodozi nvyenye viambato vyenye sumu vilivyopigwa marufuku.
Alisema kuwa Mamlaka hiyo ililiindesha msako katika maeneo mbalimbali baada ya kubaini kuwa vipodozi vinavyoingizwa kwa njia isiyo halali licha ya jitihada za kuvikamata na kuviteketeza kwa moto lakini vinaendelea kuuzwa madukani kwa kificho kutokana na kuwepo na soko la uhakika kwa watumiaji bila kufahamu madhara yake.
Alisema kuwa Mamlaka hiyo imeanzisha mkakakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi pamoja na vyuo ili kupanua wigo wa uelewa kuhusu madhara hayo kwa kuwa makundi hayo ambayo baadhi yao wameanza kutumia vipodozi hivyo kwa kufahamu ama kutofahamu madhara.
“Tumeamua kutoa elimu kwa Wanafunzi hasa ngazi ya msingi,Sekondari na vyuo vya elimu ya juu kwani nao wamekuwa wakitumia vipodozi vyenye viambata na sumu ambapo madhara yake huonekana baada ya kutumia kwa muda mrefu ili wapate kutambua na kufanya maamuzi makini wakati wa kununua na kutumia vipodozi” alisema Harananga.
Aliongeza kuwa mamlaka ya chakula na dawa imekumbwa na hali ya wasiwasi kwa baadhi ya wafanyabiashara pamoja na wajasiliamali kwa kuibua mbinu mpya kutumia lugha za ushawishi kwa watumiaji na kukimbizia sokoni vipodozi kwa kutangaza kuwa vinatengenezwa kwa kutumia mimea ya asili na kwamba havina madhara huku vikiuzwa kwa kificho bila kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara wala kibali kutoka TFDA.
Akitolea mfano vipodozi vilivyoandikwa zoa zoa na vingine vimeandikwa habari ya mjini vimetengenezwa kwa mimea ya asili na lugha za mvuto eti vinarudisha maumbile au maungo ya binadamu kuwa na mvuto kuwa hazina vigezo hivyo watumiaji wajihadhari.
Akitoa ufafanunuzi amevitaja viambato kumi na moja vyenye sumu vilivyopingwa marufuku hivyo watumiaji kuwa makini wanaponunua vipidozi hivyo vyenye madhara kwa afya ya binadamu kuwa ni Bithionol, Hexachlophene, Zebaki (Mercury) Vinyl Chloride, Ziconium, Halogenated Salicylanilide, Chloroquinenone, Hydroquinone, Steroids, Chroloform, Chlorofluorocaborn, pamoja na Methylene Chloride ambapo madhara yake huleta magonjwa ya kansa ya figo, mapafu ngozi,ubongo muwasho, mabaka meupe na meusi, chunusi, na endapo mtumiaji atapata jeraha kidonda cha upasuaji hakitapona,vile vile kwa mama mjamzito akitumia vipododi nyenye viambata vya Zebaki mtoto huzaliwa akiwa na mtindio wa ubingo.
Wakizungumza kwa niaba ya wenzao wanafunzi Dianarose Aloyce, Tami Moses na Endrew Dainiel Wakihojiana na mwandishi wa habari hizi baadhi ya wanchuo chuo cha veta baada ya kupata elimu hiyo wamekiri kuwa wao pia wamekuwa wakitumia vipodozi hivyo bila kujua madhara yake na kwamba wamekuwa wakitumia kwa kufuata mkumbo bila kujua madhara ili kuonekana warembo na watanashati.
Aidha wameongeza kuwa sehemu kubwa na wengi wao wanatumia vipodozi hivyo kwa kuiga mkumbo ili kuonekana nadhifu na watanashati pasipo kujua madhara ambayo wanaweza kuyapata kwa kutumia madawa hayo.
No comments:
Post a Comment