Kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1)(b) na Ibara ya 78 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Yanzania ya mwaka 1977 ikisomwa kwa pamoja na kifungu cha 86A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343, Yume imepewa Mamlaka ya kutangaza Viti Maalum vya Wabunge wanawake visivyopungua asilimia 30 ya Wabunge wote.
Kwa mujibu wa Uamuzi wa Serikali wa mwaka 2010 idadi ya Wabunge Wanawake wa Viti Maalum iliongezwa na kufikia asilimia 40. Katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 1015 Viti Maalum ni 113 kutokana na kuwepo kwa majimbo 8 ambayo hayakufanya uchaguzi mgawanyo wa Viti Maalum kwa sasa ni 110. Viti 3 vilivyobaki, Vitagawanywa baada ya kufanyika kwa uchaguzi katika majimbo hayo.
Vyama ambavypo vimekidhi vigezi hivyo vya Kikatiba na Kisheria vya kupata angalau 5% ya Kura zote halali za wabunge ni:
CCM VITI 64
CHADEMA VITI 36
CUF VITI 10
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jaji mstaafu
Damian Lubuva akifafanua jambo jijini Dar es Salaam jana, wakati wa kutangaza viti
maalum vya wabunge wanawake. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Emmanuel
Kawishe. Jaji Lubuva alifafanua kuwa CCM imepata viti 64, CHADEMA viti 36 na CUF imepata viti 10. (Picha na Francis Dande)
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jaji mstaafu
Damian Lubuva akifafanua jijini Dar es Salaam jana, wakati wa kutangaza viti
maalum vya wabunge wanawake. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Emmanuel
Kawishe. (Picha na Francis Dande)
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jaji mstaafu
Damian Lubuva akitanaza viti
maalum vya wabunge wanawake. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Emmanuel
Kawishe. (Picha na Francis Dande)
No comments:
Post a Comment