Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeandikisha wakulima wa Korosho
zaidi ya 300 mkoani mtwara kwenye kampeni ijulikanayo kama NSSF Kwanza
ambayo ilifanyika mahususi ili kuwafikia watu ambao wako kwenye sekta
isiyo rasmi.
Kampeni hiyo yenye malengo ya
kufikia umma wa Watanzania ambao haujafikiwa na elimu ya Hifadhi ya
jamii, Kuwaandikisha kujiunga na NSSF ili kuongeza wigo wa wanachama na
pia Kupata mrejesho wa huduma zetu kutoka kwa wanachama wa mfuko.
Imemaliza mkoani Mtwara na itaendelea kwenye mikoa mingine.
NSSF inaendelea kuwasihi Watanzania waendelee kujiunga na NSSF.
Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (wa pili kulia), akiwapa maelezo kuhusu
huduma zitolewazo na NSSF wakulima wa Kijiji cha Msijute, Kata ya Mayanga,
mkoani Mtwara, kwenye kampeni maalumu ijulikanayo kama ‘NSSF Kwanza’, ambayo
inaendelea kwa kuwafikia watu walio kwenye sekta binafsi. (Na Mpiga Picha Wetu).
Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akiwapa maelezo wakazi
wa kijiji cha Msijute jinsi ya kujiunga na Huduma ya mafao ya Matibabu
bure kwenye kampeni maalumu ya kuwaelimisha wakazi wa Mkoa wa Mtwara
juu ya faida za Hifadhi ya Jamii kupitia NSSF.
Wakazi wa Kijiji cha Msijute kata ya Mayanga Mkoani Mtwara
wakijiandikisha NSSF ili kuweza kujipatia mafao bora kutoka NSSF
yakiwemo mafao ya matibabu bure kwa wanachama na familia zao.
No comments:
Post a Comment