Tingatinga likibomoa nyumba zilizojengwa katika eneo la Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam jana. Bomoabomo kama hii imewakumba wakazi wa mji wa Dodoma na kuwaacha wakiwa hawana makazi. (Picha na Loveness Bernard)
DODOMA, Tanzania
JUMLA ya Nyumba na mapagale 180 yamevunjwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), kutokana na uvamizi na kujenga bila kufuata sheria za mipango miji.
DODOMA, Tanzania
JUMLA ya Nyumba na mapagale 180 yamevunjwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), kutokana na uvamizi na kujenga bila kufuata sheria za mipango miji.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo, Angela Msimbila, alisema lengo la kubomoa nyumba hizo ni kuwataka wananchi kujenga kwa kufuata taratibu wa mipango miji.
"BAADHI ya watu hao wamebomolewa kutokana na kuvamia na kujenga katika maeneo ya watu wengine ambao wamiliki halali, ambao wana vibali halali.
"Tumebomoa Dachi B Centre nyumba na mapagale 177 lakini nyumba 27 ndizo zilikuwa na watu ndani, pia kulikuwa na hayo mapagale ambayo yalikuwa yametegeshwa ambayo ni ya nyumba za udongo, na nyumba moja tu ndo ilikuwa ya matofali ya saluji ,"alisema Angela.
Alisema hatua hiyo itasaidia kukomesha vitisho kwa wamiliki halali wa maeneo hayo, ambavyo wamekuwa wakifanyiwa na wavamizi hao wa ardhi.
"Kuna watu ambao walikuwa na barua ambazo zinawatambulisha kuwa wao ni wamiliki halali wa viwanja, lakini wanashindwa kuviendeleza viwanja vyao kutokana na wavamizi kuvamia maeneo yao,"alibainisha Angela.
Alitaja maeneo mengine ambako bomoboa hiyo ilifanyika kuwa ni Chinangali ambayo nyumba mmoja ilibomolewa, ambayo ilikuwa na flemu za maduka matatu na uzio ambavyo vyote hivyo vilijengwa bila kufuata taratibu.
Nyumba nyingine ilivunjwa katika eneo la Barabara ya Bahi ambapo sababu kubwa ya kubomolewa huko kumetokana na holela usiyofuata maelekezo ya mipango miji.
Angela alitoa wito kwa wakazi wa mji huo kuacha tabia ya uvamizi wa ardhi, na badala yake wafuate utaratibu sahihi wa ujenzi kwa kutumia maelekezo ya ramani za ujenzi wanazopewa na siyo vinginevyo.
Angela, alisema zoezi hilo ni endelevu katika maeneo yote, kuwataka wakazi wa mji huo kufuata fuate taratibu na sheria ambapo pia CDA imetoa notisi kwa watu wote waliyovamia ardhi isiyo wahusu, ili waweze kuondoka katika maeneo hayo.
Polisi wasimamia kazi ya Bomoabomoa
Kazi hiyo iliendeshwa na mamlaka hiyo kwa kushirikiana na jeshi la Polisi ambapo wananchi wamelalamikia hatua hiyo na kudai kuwa hawakupewa muda ili waweze kuondoka.
Vilio vyatawala
Wananchi waliokumbwa na mkasa huo waliangua vilio kutokana na kubomolewa nyumba zao.
Akizungumzia hali hiyo, Mmoja wa wananchi hao, Mwajuma Hamis, alisema zoezi hilo limekuwa la kushtukiza na hawaelewi wanakwenda kujistiri wapi kwani wameshtukizwa.
Mwajuma, vitendo vya kinyama kama hivyo mara nyingi vimekuwa vikichangia kudidimiza kimaendeleo ya watu wanyonge kama wao.
I am really impressed with your writing skills and also with the layout on your weblog.
ReplyDeleteIs this a paid theme or did you customize it yourself?
Anyway keep up the excellent quality writing, it's rare to see a nice blog like this one nowadays.