HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 02, 2015

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD Awatembela Wananchi wa Jimbo lake wa Maeneo ya Masumbani, Chumbuni Kiungani na Chumbuni, Waliopata Athari za Mvua za Vuli Zinazoendelea Kunyesha Zanzibar

Mbunge wa Jimbo la Chumbini Zanzibar Mhe Usssi Salum Pondeza AMJAD akiwatembelea Wananchi wake waliopata madhara ya kuingiliwa na Maji katika Nyumba zao wakati wa mvua za Vuli zilizonyesha hivi karibu akiwa na Sheha wa Shehia ya Masumbani wakikagua maeneo hayo.
Mbunge wa Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akipata maelezo ya moja wa mtaro wa maji machafu unaosafirisha maji ya mvua katika Shehia ya Masumbani ambao huzidiwa na maji na kujaa hahi kufikia katika makaazi ya Wananchi wa Shehia hiyo.
Mhe Mbunge akiwa katikac ziara ya kutembelea maeneo ya Jimbo lake ambalo wakaazi wake wameingilia na maji wakati wa mvua ilionyeshi hivi karibuni na kuagalia jinsi ya kuufanyia mategenezo kuweza kupitisha maji na kuondoa Tatizo la kujaa kwa maji wakati wa mvua katika eneo hilo la masumbani Jimbo la Chumbuni Zanzibar.
Sheha wa Shehia ya Masumbani akimuonesha maeneo yanayojaa maji wakati wa Mbunge wa Jimbo hilo alipowatembelea Wananchi wake waliopata madhara ya kuingiliwa na maji ya mvua majumbani kwao. 
Mbunge wa Chumbuni akiwa katika ziara ya kutembelea Wananchi wake Jimboni kuwafariji.akiwa na Viongozi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akimsikiliza Sheha wa Shehia ya Masubani wakati wa ziara yake kuwafariji Wananchi wa Jimbo lake walioingiliwa na Maji wakati wa Mvua hivi karibuni. 
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwagaia pipi watoto wa madrasa ya masumbani wakati wa ziara yake katika Jimbo lake kuwafariji Wananchi walioingiliwa na maji majumbani mwao.

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe. Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwafariji Wananchi wa Jimbo lake waliopata madhara ya mvua za vuli kuingiliwa na maji katika makaazi yao, na kutoa msaada kwa Wakaazi hao.  
Wananchi waliopata madhara ya mvua za vuli wakimsikiliza Mbunge wao alipofika kuwatembelea na kuwafariji na kuwakabidhi msaada. 
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Pondeza AMJAD, akimkabidhi msaada wa vyakuma mmoja wa Mwananchi wa Jimbo lake Shehia ya Karakana waliopata maafa hayo ya mvua hivi karibu. 
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Pondeza AMJAD, akimkabidhi msaada wa chakula mmoja wa Mwananchi wa Jimbo lake Shehia ya Karakana waliopata maafa hayo ya mvua hivi karibu. 
Mbunge wa Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akimsikliza Mwananchi wa jimbo lake wakati alipofika kuwatembelea Wananchi wa Jimbo hilo waliopata maafa ya kuingiliwa na maji katika majumba yao eneo la masumbani Zanzibar.
Mbunge wa Chumbuni akiwa Watoto wa Shehia ya Masumbani akiwagaia peremende, wakati akiwa katika ziara yake.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe. Ussi Salum Pondeza AMJAD akitembelea Shehia ya Charakana ilioko katika jimbo lake kuwafariji Wananchi waliopata maafa ya mvua za vuli zinazonyesha katika visiwa vya Unguja.
Mbunge wa Chumbuni Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwa katika ziara yake katika Shehia ya Karakana kuwatembelea Wananchi wa Jimbo lake waliopata maafa ya mvua za Vuli.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akipata maelezo kutoka kwa Sheha wa Karakana wakati wakiwa katika eneo linaliothirika kwa kujaa maji wakati wa mvua ikinyesha na kuahidi kulichukulia hatua ya kuchimbwa kwa mtaro mkubwa wa maji kuweza kupitisha maji hayo wakati wa mvua ikinyesha. kuondoa kero za Wananchi wa eneo hilo.
Sheha wa Shehia ya Karakana akiwa na Mbunge wa Jimbo la Chumbuni akitembelea maeneo yaliopata madha ra kujaa maji wakati wa mvua za vuli zinazonyesha na baadhi ya Wananchi wa Jimbo hilo kuingilia na maji makaazi yao. 
Mbunge wa Chumbuni akitembelea Maeneo ya Karakana yaliojaa maji.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspots.
Zanzinews.com 

No comments:

Post a Comment

Pages