Waliokuwa maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
wakitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam jana baada
ya kufikishwa mahakamani hapo kwa kosa la uhujumu uchumi na kutoa makontena 329
bandarini bila ya kulipiwa kodi na kuisababishia serikali hasara ya Sh. Bilioni
12.7. (Picha na Francis Dande).
Aliyekuwa Kamishna wa Kodi
na Forodha wa TRA, Tiagi Masamaki, akiingia
katika gari lenye namba za usajili T 442 BBL wakati alipofikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana kwa kosa la uhujumu
uchumi na kutoa makontena 329 bandarini bila ya kulipiwa kodi na kuisababishia serikali
hasara ya Sh. Bilioni 12.7. Kushoto ni mtuhumiwa mwingine, Harun Mapande,
ambaye alikuwa Mkuu wa Mfumo wa Kompyuta TRA.
Aliyekuwa Kamishna wa Kodi
na Forodha wa TRA, Tiagi Masamaki, akiingia
katika gari.
Tiagi Masamaki, akiwa na watuhumiwa wenzake.
Mkuu wa Mfumo wa Kompyuta wa TRA, Harun Mapande akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi wakati akisubiri kupelekwa katika mahabusu ya gereza la segerea baada ya kusomewa mashtaka yao.
Na Dotto Mwaibale
KASI ya utendaji kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa Kasim Majaliwa imeanza kuwagusa baadhi ya watendaji wa Serikali baada ya maofisa wanane wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akiwemo Kamishna wa Forodha wa mamlaka hiyo Tiagi Masamaki (56) kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutoa makontena 329 bandarini bila ya kulipiwa kodi na kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 12.7.
Ukimuondoa Masamaki maofisa wengine waliopandishwa kortini ni Habibu Mponezya (45) Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja,Bulton Mponezya (51)
Wakili wa Serikali Mwandamizi Christopher Msigwa akisaidiana na Peter Vitalis ameadi leo mchana mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa makosa mawili.
Alidai makosa mawili ya uhujumu uchumi ni kula njama ya kuidanganya Serikali na kuisababishia Serikali hasara. Kesi hiyo ni namba 35/2015 ya uhujumu uchumi.
Ilidaiwa katika shtaka la kwanza katika tarehe tofauti kati ya Juni 1 na Novemba 17 mwaka huu, sehemu isiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama ya kuidanganya Serikali kuwa sh. bilioni 12.7 zimetolewa kwa kutoa makontena 329 katika Bandari Kavu ya Azam, baada ya kodi zote kutolewa.
Katika shtaka la pili, washtakiwa wanatuhumiwa katika ya Juni Mosi na Novemba 17 mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam walishindwa kutimiza majukumu yao kwa namna inavyotakiwa na kusababisha Serikali kupata hasara ya sh. bilioni 12.7.
Baada ya washtakiwa hao kusomewa makosa yao, Hakimu Shahidi aliwaeleza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo hawatakiwi kujibu chochote kama kweli au si kweli.
Aliongeza kuwa Mahakama Kuu ndiyo inamamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo kama wanataka dhamana wapeleke maombi ya dhamana katika mahakama hiyo.
"Kama mnataka dhamana pelekeni maombi Mahakama Kuu kwa sababu mahakama hii hawezi kutoa dhamana," alisema Hakimu Shahidi
Hata hivyo, upande wa utetezi ulidai kuwa kesi hiyo ifikishwa mahakamani hapo bila kibali na pia waliomba mshtakiwa namba nne Mrema anamtoto mchanga kwa hiyo wanaiomba mahakama imfikirie.
Wakili Msigwa alidai upelelezi bado unaendelea, wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Kesi hiyo itatajwa Desemba 17 mwaka huu kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika.

No comments:
Post a Comment