Aliyekuwa Kocha
Mkuu wa timu ya soka ya wanawake, Twiga Stars, Rogasian Kaijage, akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu kujiuzulu kwake rasmi
kuifundisha timu hiyo. (Na Mpiga Picha Wetu).
DAR ES SALAAM, Tanzania
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga
Stars), Rogasian Kaijage amejiuzulu nafasi hiyo kuanzia leo baada ya
kuomba kwa uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).
Kaijage aliiongoza Twiga Stars kwenye fainali za michezo ya Afrika
(All Africa Games) zilizofanyika nchini Congo Brazzavile Septemba mwaka
jana, baada ya kuiondoa timu ya taifa ya Zambia katika hatua ya mtoano.
TFF imesikitishwa na taarifa za kujiuzulu kwa kocha huyo mwenye
leseini A ya CAF, ambaye amekuwa akizinoa timu za taifa za wanawake ya
wakubwa (Twiga Stars) pamoja na timu ya wanawake wenye umri chini ya
miaka ya 20 (Tanzanite) tangu mwaka 2013.
Kufuatia kujiuzulu kwa kocha Kaijage, TFF inaendelea na programu za
maendeleo ya soka kwa wanawake, ikiwemo kuendesha ligi ya wanawake
(Tanzania Women League).
TFF inamtakia kila la kheri kocha Rogasian Kiajage katika shughuli zake.
Aidha maandalizi ya mchezo kati ya Twiga Stars dhidi ya Zimbambwe
yataendelea chini ya kocha atakayeteuliwa kuchukua nafasi yake, mchezo
utakaochezwa mwezi Machi mwaka huu na mshindi kucheza na Zambia.
TFF itaendelea kupambania kwenye maendeleo ya soka la wanawake.
No comments:
Post a Comment