HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 07, 2016

BANK M TANZANIA YATOA RIPOTI YA FEDHA YA MWAKA 2015

Ofisa Mtendaji Mkuu Biashara wa Benki M Tanzania, Jacqueline Woiso, akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati akitoa ripoti ya fedha ya mwaka 2015. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa benki hiyo, Allan Msalilwa. (Picha na Francis Dande)

DAR ES SALAAM, Tanzania


KUPANDA kwa kasi kwa viwango vya kubadilishia fedha   imekuwa ni  tatizo kutokana na bank kushindwa kufikia malengo yake kwa wakati.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wakutoa ripoti yarobo ya tatu ya  mwaka 2015 Mkurugenzi Mkuu wa Bank M, Jacqueline Woiso alisema wamefanikiwa kutoa mikopo katika sekta mbalimbali.

Alisema wametoa mikopo kwenye sekta ya viwanda na uzalishaji,biashara, ujenzi, mawasiliano pamoja na kilimo kwani  wametambua umuhimu wa sekta hizo.

 Owiso alisema faida kwa bank hiyo imeomgezeka kufikia sh 23.66 Bill mwisho wa mwezi desemba 2015 ikilinganishwa na 17.89 bill za mwaka 2014.

Alisema wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwa na wafanyazi asilimia hamisi  kwa hamsini kati ya wanawake na wanaume.
Hata hivyo alisema rasulimali za bank hiyo zimeongezeka sh 689.35 bill kwa mwaka 2014 na kufikia sh 861.94 bill mwishoni mwa mwaka jana .

No comments:

Post a Comment

Pages