WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh.
Profesa Makame Mbarawa amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Mhandisi George Sambali kukaimu nafasi ya
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kufuatia kifo
cha aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo,
Mhandisi Suleiman S. Suleiman.
Mhandisi
Suleiman alifariki dunia tarehe 18 Januari, 2016 wakati akipelekwa katika
hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam baada ya kuishiwa nguvu ghafla akiwa katika
mazoezi ya kuogelea katika eneo la
Feri, jijini Dar es Salaam.
Akitangaza
uteuzi huo kwa niaba ya Waziri Mbarawa
mbele ya Menejimenti ya TAA Jumatano tarehe 20 Januari, 2016 katika Ofisi za
Makao Makuu ya Mamlaka hiyo kwa niaba ya Mh. Waziri, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard
Chamuliho, alisema uteuzi wa
Mhandisi Sambali umeanza rasmi tarehe 20 Januari, 2016.
Mhandisi
George Sambali alizaliwa mwaka 1965, mkoani Tabora na ana shahada ya Uzamili ya
Sayansi Uhandisi Uchukuzi na Barabara (MSc. Transportation (Transport &
Road) Engineering, aliyoipata mwaka 1999- 2001 nchini Uholanzi.
Mhandisi
Sambali alihitimu shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Uhandisi Ujenzi (BSc.Civil Engineering) katika Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1995.
Mhandisi
Sambali pia amepata mafunzo na kozi mbalimbali za masuala ya anga kutoka
katika vyuo vya hapa nchini na nje ya
nchi, ikiwemo Stashahada ya Uongozi wa
Viwanja vya Ndege (Certificate in Airport Executive Leadership) mwaka 2014 huko
Montreal, Canada.
Pia
mwaka 2015 alitunukiwa Stashahada ya Wataalamu wa Kimataifa wa Viwanja vya
ndege (Post-Graduate Diploma in International Airports Professionals (AIP)
chini ya AMPAP nchini Canada.
Mhandisi
Sambali aliajiriwa na TAA mwaka 2001 kama Meneja Mipango, Usanifu na Uthamini
(Manager Design, Planning and Evaluation) na mwaka 2012 aliteuliwa kuwa Kaimu
Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi na Ufundi.
Mwaka 2013, Mhandisi Sambali aliteuliwa kuwa
Mshauri Maalum wa Mkurugenzi Mkuu kabla ya mwishoni mwa mwaka jana kuteuliwa
tena kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Mhandisi
Sambali ni mwanachama kwenye vyama mbalimbali vya kitaaluma kikiwemo cha
Wataalamu wa Kimataifa wa Viwanja vya Ndege chini ya Baraza la Viwanja vya Ndege Duniani (ACI) na
Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga
(ICAO).
Pia
Mhandisi Sambali ni Mjumbe wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET); Mjumbe
katika Jukwaa la Kimataifa la Uendeshaji wa Uchukuzi Vijijini (IFRTD); na Bodi
ya Usajili wa Wahandisi (ERB).
IMETOLEWA NA KITENGO CHA SHERIA NA
UHUSIANO –TAA Januari 25, 2016
No comments:
Post a Comment