Na Mwandishi Wetu, UKEREWE
VIKUNDI vya Wazee wa
Mamba 'Wanauame' na Hapa Kati tu Wanawake, vya mkoa wa Michezo wa Ukerewe, vimevunja rekodi ya mashindano ya mbio
za Mitumbwi za Balimi Boat Race 2016 na kutwaa ubingwa na kujinyakulia vikombe
medali za dhahabu na fedha taslimu sh.2.2.
Mashindano hayo
yalifanyika juzi kwenye ufukwe wa Monarch hoteli wilayani Ukerewe, ambapo mgeni
rasmi Mkuu wa wilaya hiyo, Josephat Mkirikiti alikabidhi zawadi kwa washindi wa
mivhuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Bia nchini (TBL) kupitia bia ya
Balimi Extra Lager.
Bingwa wa mashindano
hayo kwa upande wa wanaume, kikundi cha Wazee wa Mamba kilitumia dakika 31
kuweza kutwaa ubingwa huo na kukabidhiwa kombe,medali za dhahabu na fedha
taslimu, sh.1.2 ,huku Kikundi cha Hapa Kazi tu kwa wanawake,kiling’ara kwa
kushika nafasi ya kwanza, kikitumia dakika 39 na kukabidhiwa fedha taslimu sh.
1,000,000,medali za dhahabu na kombe.
Nafasi ya pili kwa wapiga makasia
hao kwa wanaume ilikwenda kwa kikundi cha Kama Ipo Ipo tu kwa kutumia dakika 34
na kujinyakulia kitita cha sh.1,000,000, kikundi cha Ya Mtoto kilinyakua nafasi ya tatu baada ya kutumia
dakika 35 na kulamb sh.800,000 na nafasi
ya nne ilinyakuliwa na kikundi cha Tuliochelewa ambacho kiliondoka na sh.600,000.
Vikundi vya Usipoteze muda, Nani
Kaona,Maisha ni kutafuta ,Mbeya City, Hapa Kazi tu na Ole wenu,vilivyoshika
nafasi ya tano hadi ya kumi,kila kimoja kilipata kifuta jasho cha sh.250,000.
Kwa upande wa wanawake,nafasi ya
pili ilikwenda kwa kikundi Kaza Roho,ambacho kilitumia dakika 41 na kikapata
sh.800,000, kikundi cha tatu cha Kazi na
Malengo, kilitumiaz dakika 43 na kubeba sh.600,000 na nafasi ya nne
ilichukuliwa na kikundi cha Upendo na kuzawadiwa sh.400,000.
Hata hivyo katika mashindano hayo
kikundi cha nahodha Yasinta kutoka Kirumba mtumbwi wazo ulipinduka na kuzama
lakini baada ya kuokolewa walibadili mtumbwi na kuendelea mashindano na
ukashika nafasi ya tisa.
Vikundi vitatu vy tabia Njema,
Mtafuta cha Uvunguni na Eberneza vilivyoshika nafasi ya tano hadi ya saba
walifutwa jasho kwa sh.200,000 kila kimoja, hata hivyo vikundi vitatu
viliondolewa kwenye mashindano hayo baada ya kubainika vilishiri mashindano kama
hayo kwenye mikoa ya Mara na Mwanza, kimoja kikikishika nafasi ya kwanza na
kingine nafasi ya pili.
Akizungumza wakati akikabidhi
zawadi, Mkuu wa Wilaya, Mkirikiti, alisema kampuni ya TBL isichoke kupeleka
mashindano kama hayo wilayani humo kwa sababu wananchi wake wanapenda michezo
na burudani.
“TBL niwapongeze mnafanya vizuri
katika eneo la kodi,mmekuwa marafiki wa Uerewe sababu mmetufanya tuwe sehemu ya
maisha yenu.Changamoto yenu mtuangalie katika sekta za afya na elimu (madawati).Mtusaidie
hili la madawati na tupo tayari kuondoa vikwazo vinavyowakwaza ili tuondokane na kero ya madawati,”alisema
Mkirikiti.
Pia, aliipongeza kampuni hiyo kwa
kuwaondoa washiriki (mamluki) waliokwisha shiriki mashindano hayo mikoa mingine,ambo
walikuja kuchukua nafasi zizizo za kwao na katika eneo lisilo la kwao.
Aidha, Meneja Mauzo wa TBL Kanda ya
Ziwa, Godwin Zacharia,alisema lengo la TBL kwa miaka 16 ya mashindano ya
Balimi, ni kukuza utamaduni na michezo ukiwemo wa kupiga makasia .
Alisema, kutokana na kukubaliwa na
jamii ya Kanda ya Ziwa,wataendelea kuyaboresha kwa kuongeza zawadi na washiri kila
mwaka kwa sababu bado wana kiu na kuahidi kushughulikia changamoto ya washiriki
bandia .
Aidha, Mwenyekiti wa Chama cha
Mitumbwi Taifa-Tanzania Canoe Assocition,(TCA) Richard Mgabo alisema kuwa, akiwa
mwasisi wa mashindano ya makasia,anafarijika kuona mchezo huo ambao haukuwepo
nchini, ukipata mashabiki na kuzidi kupendwa na wananchi wa kada mbalimbali na
kuishukuru TBL kwa udhamini wao tangu yaanzishwe.
Mashindano hayo Balimi Boat
Race yamefikisha umri wa miaka 16 tangu
yaanzishwe mwaka 2000, kwa udhamini wa TBL kupitia kinywaji chake cha bia ya
Balimi Extra Lager,ambapo mwaka huu Ukerewe yamefanyika kwa hadhi ya kimkoa baada
ya wilaya hiyo kupewa hadhi ya mkoa.Fainali ya mwisho itafanyika Januari 30,
mkoani Geita.
No comments:
Post a Comment