HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 16, 2016

KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHA KURASINI CHAPATA MSAADA





UN Clubs Tanzania Network kanda ya Dar es Salaam wakishirikiana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako wametoa msaada kwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Kurasini kwenye siku ya wapendanao ili kuonesha upendo mkubwa kwa watoto hao. Vijana hao wa UN Club Tanzania Network wanafanya kazi siku ya wapendanao nchi nzima za kusaidia jamii na vijana wa jijini Dar es salaam wameungana na watoto wa kituo cha Kurasini kwa kutoa msaada na wanafunzi hao wametoka katika shule za sekondari za Zanaki, Azania, Benjamin na Jangwani. Akizungumzia msaada huo, Afisa Ustawi wa Jamii katika kituo hicho. Jack Omary aliwashukuru kwa kuwatembelea siku ya wapendanao maana kuna watu wengine wanaitumia siku ya wapendanao kwenye starehe na hata kutumia pesa bila kuangalia kuna watu wanahitaji msaada. Nae Stella kutoka UN Clubs Tanzania amesema lengo la kuja katika kituo cha watoto yatima cha Kurasini nikujumuika na hao watoto ambao hawana wazazi na pia watoto wenye shida mbalimbali.
Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (kulia) akimkabidhi msaada kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto Bi. Jack Omary(kushoto) ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii kituo cha taifa cha kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kurasini, hafla hii imefanyika katika siku ya wapendanao. Misaada hyo imetolewa na vijana wa UN Clubs Tanzania Network kwa kanda ya Dar es salaam pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako. (Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog).
Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (kushoto) akiwakabidhi misaada watoto wa Kituo cha Kurasini, katikati ni mtoto Aboubakary Seif ambaye alipokea kwa niaba ya watoto wenzake.
Zuwena (kushoto) akimkabidhi mpira mtoto aliyewawakilisha wenzake kituoni hapo.
Mwenyekiti wa Jangwani Fema, Jeniffer Kayombo akiwaasa watoto kusoma kwa bidii ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Pages