Picha Wanawake Kutoka Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha Pamoja na Viongozi na Wakufunzi Kutoka Tasisis ya Manjano Foundation Wanaoudhuria Mafunzo ya Ujasiriamali Kutoka Taasisi ya Manjano Foundation.
Awamu ya Sita ya Mafunzo ya Ujarisiamali kwa Mkoa wa Arusha yameanza leo. Wanawake 30 wa jiji la Arusha Watanufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yanayoendeshwa na mtaalamu wa mambo ya Biashara Bw Alphonce Masagga na mama Shekha Nasser. Mafunzo haya yenye lengo la kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya Tasnia ya urembo. Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Golden Rose Hotel, Jijini Arusha.
Mafunzo haya yamegawanywa katika Sehemu mbili ili kumsaidia mjasiriamali wa kike kujikwamua. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali fedha na muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake.
Awamu ya pili mshiriki anafundishwa matumizi sahihi ya vipodozi kuendana na wakati, mfano office makeup, day makeup, evening na namna ya kumpamba bi harusi. Pia wanafundishwa namna bora ya kutumia vipodozi vya LuvTouch Manjano kwa lengo ya kuwa kila mshiriki atakayehitimu mafunzo haya aweze kujiajiri na kujitegemea kwa kuendesha maisha yake ya kila siku kwa kuwapambamba watu wenye shuguli mbalimbali.
Pamoja na mafunzo, kila mshiriki anaunganishwa na mwanamke mmoja mwenye mafanikio katika biashara au uongozi katika jamii kwa lengo la kumuongoza katika safari yake ya biashara kwa muda wa mwaka mzima.
Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa mikopo kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea
No comments:
Post a Comment