Msanii Eliabeth Michael Lulu akiwasili kutokea nchini Nigeria akiwa na Tunzo yake mkononi ambayo alishinda nchini Nigeria katika Mashindano ya Africa Magic Viewers Choice Awards 2016 katika Kipengele cha Filamu Bora ya Afrika Mashariki kupitia filamu yake ya Mapenzi ya Mungu ambayo ipo chini ya Kampuni ya Mahiri ya utengenezaji na usambazaji wa Filamu ya Proin Promotions Ltd.
Akiwaaga mashabiki wake na wapenzi waliokuwa uwanja wa ndege wa Mwl Nyerere jijini Dar Es Salaam mara baada ya kuwasili kutokea Nchini Nigeria ambapo alikwenda kushiriki Mashindano ya Africa Magic Viewers Choice Awards 2016 na kuibuka kidedea
Msafara wa Lulu ukiondoka Uwanja wa Ndege kuelekea Escape one ambapo baadhi ya wapenzi na mashabiki waliweza kumpongeza kwa ushindi ulioipatia Taifa la Tanzania Sifa katika tasnia ya Filamu.
Msafara wa kuelekea Escape.
Msanii Elizabeth Michael almaarufu Lulu akiwapungua watanzania wakati akielekea Escape one mara baada ya kuwasili kutoka Nchini NIgeria.
Akiwapungia mkono watanzania waliokuwa katika kituo cha daladala cha Buguruni.
Bodaboda wakiongea na Lulu wakati akielekea Escape One.
No comments:
Post a Comment