HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 10, 2016

UGONJWA WA KIPINDUPINDU WAINGIA ZANZIBAR

Na Talib Ussi, Zanzibar

Wananchi wa Zanzibar wametakiwa kuchukua tahadhari kutokana kuibuka upya ugonjwa wa Kipindupindu baada ya mvua kuza kunyesha ndani ya siku mbili.

Akitoa tamko hilo Daktari dhamana Unguja Fadhil Mohammed alisema kwamba wagonjwa 33 wamelzwa katika kambi maalum za wagonjwa hao zilioko Chumbuni Wilaya Mjini 31, Ukongongoroni Wilaya ya kati mmoja na Fujoni Wilaya ya kati mmoj kuazia Jumanne.

“Maradhi ya kipindupindu yapo wananchi mnatakiwa kuchukua tahadhari kubwa kutokana kasi ya ugonjwa huu” alisema Mohammed.

Alisema sababu ya maradhi hayo ya mripuko ni kutona kuenea kwa uchafu katika mitaa mingi ya Zanzibar jambo ambalo linaathiri wanachi sasa.
Alisema tokea Septemba mwaka jana wagonjwa 1974 wametibiwa na kati yao 22 walifariki kutokana na maradhi hayo.

Ali Juma ambaye ni mkurugenzi wa maafa Zanzibar alisema utupaji wa vitu ovyo katika masalio ya maji imepeleke mvua zinaponyesha kuwepo kwa ucahfu mwingi.

“Watu wetu wamezoea kutpa ovyo ovyo manepi na Penpasi pasina kuzingatia kwamba lile linaweza kuwaathiri baadae” alisema Juma.

Alisema dini zoote zinahimiza usafi kwa hiyo aliwataka wananchi kuweka usafi katika maeneo yao na kuwa waangalifu na watoto wasichezee vitu vilivyooza.

Alifahamisha kuwa changamoto kubwa wanayoipata katika kupambana na maradhi hayo ni kuwepo katika maeneo tofauti visiwani humu.

“Tuweni makini zaidi na watoto wetu kwani wao huchezea kila kitu bila ya kujua kwamba wanaweza kuathirika” alieleza Juma.

Kutokana na suala hilo alivitaka vyombo vya habari kuwaelimisha wananchi katika kupambana maradhi hayo.

No comments:

Post a Comment

Pages