HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 10, 2016

WAKAZI WA MUHEZA KUKUTANA MACHI 12

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Muheza, Balozi Adadi Rajabu (pichani), anatarajia kukutana na wa Wakazi wa wilaya hiyo, wanaoishi jijini  Dar es Salaam kesho, kwa ajili ya kuzungumzia mipango ya utekelezaji wa maendeleo katika jimbo hilo.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Mkutano huo, Clement Mang’enya, alisema wilaya ya muheza hivi sasa imejipanga kuwasogezea maendeleo karibu wakazi wote, hata hivyo, yote hayo yatafanikiwa iwapo watakuwa msitari wa mbele  katika kutoa ushirikiano.

“Mkutano huo, utafanyika katika kijiji cha Makumbusho Kijitonyama jijini, kuanzaia saa 3 asubuhi kwa hiyo, ni fursa nzuri kwa Wanamuheza kujitokeza kwa wingi ili kuja kuwa sehemu ya watakaotoa mawazo ya nini kifanyike katika kipindi hiki cha miaka mitano ya Balozi Adadi,”alisema Mang’enya.

Alisema, katika mkutano huo mambo mabalimbali yatajadiliwa lakini kubwa litakalochuku nafasi kubwa litakuwa la kuzipatia madawati shule zote za wailaya hiyo, ili kuwaondolea adha ya kukaa chini baadhi ya wanafunzi.

“Hivi sasa tumejipanga katika kuondoa baadhi ya kero ambazo nyingine ni za miaka mingi kwa hiyo kupanga ni kuchagua hivyo basi katika miaka hii mitano tumechagua kujiletea maendeleo ambayo tumeyahitaji kwa miaka mingi,”alisema Mang’nya.

Mang’enya, alisema mkutano huo, pia utakuwa na agenda ya uhuishaji wa Mfuko wa Maendeleo wa Muheza (MTDF), lengo likiwa ni pamoja na kupata viongozi na wajumbe ambao watausimamia kwa ufanisi mfuko huo ukilinganisha na sasa.

Aidha, Mang’enya alitoa wito kwa wakazi wanaoishi katika mikoa mingine nchini kuandaa mikutano kama hiyo, yenye lengo la kusaidia jimbo lao kimaendeleo ambayo yataijengea heshima wilaya yao.

No comments:

Post a Comment

Pages