Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof Godius Khyarara ametoa rai kwa wale Wote walionunua nyumba za Mtoni Kijichi kukamilisha malipo ya nyumba hizo ndani ya siku 30 na kama hawatafanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kunyang’anywa nyumba na kuuzwa kwa wanachama wengine.
Mkurugenzi Mkuu huyo
alisema, wapo watu wameshikilia nyumba na hawajakamilisha malipo kama mkataba
unavyosema na kusisitiza kuwa ndani ya mwezi mmoja kama mtu hajakamilisha
malipo, masharti yote ya mkataba yatafuatwa.
Maagizo hayo aliyatoa wakati
alipotembelea Miradi mbalimbali ya NSSF Ukiwemo mradi wa Dege Eco Village.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (wa pili kulia), akiangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi wa nyumba za Dege Eco Village zilizopo Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara akifafanua
jambo jijini Dar es Salaam, kuhusu wateja walionunua nyumba za NSSF
zilizopo Mtoni Kijichi kukamilisha malipo yao ndani ya siku 30 kabla ya hatua
za kisheria hazijachuliwa kwa watakaoshindwa kufanya hivyo. Kushoto ni Meneja
Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo.
Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo akitoa maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa nyumba za Dege Eco Village. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Godius Kahyarara.
Baadhi ya wafanyakazi wa mradi wa ujenzi wa nyumba za Dege Eco Village.
Baadhi ya wafanyakazi wa mradi wa ujenzi wa nyumba za Dege Eco Village.
Meneja
Kiongozi Idara ya Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kulia) akifafanua jambo wakati Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara alipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za Dege Eco Village Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kulia) akiangalia moja ya nyumba zilizopo katika mradi wa Dege Eco Village.
Sehemu ya jikoni.
Sehemu ya jikoni.
Nyumba za kisasa za Dege Eco Village.
No comments:
Post a Comment