HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 01, 2016

VIONGOZI WANNE WA CUF WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI ZANZIBAR

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Viongozi  wa nne  wa Chama cha wananchi CUF Wilaya ya Magharbi (A) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi  wakihusishwa na mipango ya ulipuaji wa nyumba za Makamu Wa Pili Balozi Seif Ali Idd na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Vuai Ali Vuai.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar, Salum Msang- DCP wakati akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake Makao Makuu ya Polisi Visiwani hapa.

Alisema katika mahojiano yao ya awali watuhumiwa hao wamekiri kuripua nyumba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar na mipango yao ilikuwa ni kumalizia nyumba za waheshimiwa hao.

“Unajua hizi nyumba zote zipo katika eneo moja la kijichi Bububu kwa hiyo walikuwa wanakwenda moja baada ya nyengine” alisema Msangi.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Omar Bakar Nassor (26)mkaaazi wa Bububu Unguja, Hassan Omar Issa (67) ambaye alimtaja kuwa ni Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Magharbi, Saleh Mohammed Saleh (34) Katibu wa CUF wilaya hiyo ya Magharibi A na Suleiman Mohamed Bakar katibu wa Jimbo la Mfenesini CUF .

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa na mabomu matano ya kienyeji, ambapo alidai mtuhumiwa wa mwanzo alikiri kutupa Bomu katika Nyumba ya Kamishna akiwa na mwezake ambaye anatafutwa.

“Watuhumiwa hawa walifanya hivi ikiwa ni kkakati wa chama chao kufanya hujuma ili kujenga ghofu wananchi wasishiriki Uchaguzi wa Marejeo” alieleza Msangi.

Alifahamisha kuwa mtengenezaji wa mabomu hayo naye bado anatafutwa na kudai kwamba karibu watafanikiwa kumtia nguvuni.


Alisema kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vikosi vyengine vya usalam vimejipanga kuendeleza Doria ya kiintelijensia na operesheni ili kuwabaini wale wote wanaotenda uhalifu.

“Jeshi linatoa onyo wale wote ambao wamepanga kufanya uhalifu wakaacha kwani kuna siku watatiwa mikononi mwa Dola” alisema Msangi.

Kupitia mwanasheria wa chama cha CUF Masoud Faki Masoud alisema hawajaweza kuthibitisha viongozi wao kwamba wamekiri hivyo kwani hawako sehemu ambayo wanahojiwa.

“Tunafuatilia tuone nini kinaendelea lakini kwa sasa madai haya hatuwezi kuyaamini na tunaimani nishtuma tuu hizo” alieleza Masoud.

Wanachama wa chama cha wananchi CUF wamekuwa wakikamatwa siku hadi siku na kushtmuiwa kwa kesi uripuzi maeneo mbali mbali.

No comments:

Post a Comment

Pages