Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Muhammed Shein amesema hawako tayari kuendesha nchi kwa kupewa Masharti kutoka kwa wahisani.
Dk. Shein alieleza hayo wakati akitangaza wajumbe wa Baraza la Mapinduzi (Baraza la Mawaziri) huko Ikulu Zaanzibar ambapo amewataja mawaziri 13 na wajumbe wa wili wa baraza hilo wakiwemo wapinzani watatu.
“Hatuko tayari kuongoza nchi yetu yenye katiba yake na sheria zake kwa masharti aa fanyeni hivi na vile ili tupewa misaada hatufanyiii hata siku moja”alisema Dk. Shein.
Alisema kwamba yeye hana taarifa ya Tanzania kuzuiliwa misaada bali ni Marekani pekeyake kupitia MCC ndio wameondoa na kudai wahisani wengine wanendelea bado.
“Hata wakizuia sisi tutatafuta vyanzo vyetu wenyewe ili tuweze kujikimu kimapatoa lakini sio turidhie matakwa mabwana Fulani”alisema Rais Shein.
Alisema aliwaona Jumuiya ya Ulaya wa kisema kwamba hawajakatisha misaada ispokuwa vyombo vya habari ndio vinavyoeneza tuu uvumi huo.
Alisema kama watepewa misaada basi watapokea kama wahisani wameamua kuwanyima wala hawatawalazimisha.
Alieleza kwamba mkakati walionao sasa kupitia Serikali yake aliyounda ni kutafuta vyanzo vya kifedha ili kuondoa utegemezi.
Alisema misaada ni njia moja ya kushirikiana na alidai kwamba wakiamua kuwanyima kwa sababu ya kurudia uchaguzi wao hawana hoja kwani walilolifanya ni jambo la kisheria.
“Ikiwa wanatunyima kwa sababu tumefanya uchaguzi wa marudio basi, tutafuta vyanzo vyetu” alieleza Dk. Shein.
Alisema wataendelea kupokea na kukopo na hasa katika Bank ya Exim ya china na marafiki wengine ambao watakuwa tayari kuwakopesha, ‘ lakini wao kama hawatatupa wala hushuhuliki’.
“Kukopa ni wajibu kwa hiyo na sisi hautaona haya na wao ambao watatukopesha” alisema Dk. Shein.
Katiba.
Akizungumzia juu ya badilisha kipengele ili kuondoa serikali ya umoja wa kitaifa alisema hata badilisha kipengele chochote cha katiba ili aweze kuunda Serikali ya CCM pekee.
“Sitabadilisha kupengele hata kimoja kwenye katiba kwani kukwama si katiba bali ni maamuzi ya wananchi lakini katiba yetu iko vizuri sanaa” alieleza
Alisema kama haja hiyo iko wataamua wenyewe wananchi au baraza la wawakilishi kuona kama kuna haja au hakuna ya kubadilisha vipengele vya katiba.
Alisema tatizo sio katiba bali vyama vya siasa vya katiba kutofuata utaratibu wa tume ya Uchaguzi wa Zanzibar (ZEC).
“Katiba haina tatizo lakini CUF waliposema hawashiriki basi ndio matokeo yake hayaa lakini katiba yetu haina tatizo” alieleza Dr. Shein.
Utauzi wa Wizara
Akizitangaza wizara hizo 13 alisema ni kinyume katika Serikali iliyopita ambapo aliunda Wizara 16 alidai ameunda wizara chache kwa lengo kutaka kuona uwajibikaji na ufanisi katika kutimiza malengo waliojiwekea
Alisema katika ofisi yake atakuwa na wizara tatu ambazo ni Wizara ya Ofisi ya Rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi ambapo Waziri wake atakuwa ni Issa haji Ussi (Gavu) ambaye katika Serikali iliyopita alikuwa Naibu wa Waziri wa wizara ya Miundombinu na Mawasiliano.
Aliendelea kwa kutaja Wizara ya Ofisi ya Rais Katiba, sheria, Utumishi wa Umma na utawala bora ambapo waziri wa zamani wa wizara hiyo iliyoongezwa katiba na sheria ndiye waziri, Haruna Ali Suleiman.
Haji Omar Kheiry amendelea kushikilia Wizara yake ile ile ya zamani ambayo ni Ofisi ya Rais Tawala za mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ ambapo Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Muhammed Aboud Muhammed anaendelea.
Upande wa Wizara ya Afya aliyekuwa Naibu Waziri Mahmud Thabiti Kombo amepanda hadi kuwa Waziri wa wizara hiyo ambapo aliyekuwa Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk Khalid Salim Muhammed amekabidhiwa jukumu la Wizara ya Fedha na mipango.
Wazara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imekwenda kwa bibi Riziki Pembe Juma na Balozi Amina Salim Ali amepewa Wizara ya Biashara viwanda na Masoko.
Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Rais Dk. Shein amemteua kaka wa Rasi wa Awamu ya tano Balozi Ali Abeid Karume wakati aliyekuwa Mkurugenzi wa zamani Manispaa ya Zanzibar Rashid Ali Juma amepewa Wizara ya Habari, utalii, utamaduni na michezo.
Hamad Rashid Mohammed (ADC) ambaye aliingia Barazani kwa nafasi za Rais atakuwa Waziri wa Kilimo, Maaliasili Mifungo na Uvuvi kwa upande wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto waziri wake atakuwa Maulin Castiko.
Alimalizia Wizara ya Ardhi maji nishati na mazingira ambapo alimtaja Bi Salama Aboud Twalib ndiye waziri na kuwataja wajumbe wawili watakaoingia katika baraza la Mapindu (mawaziri wasio na wizara maalum) ambao ni Said Sudi Said wa AFP na Juma Ali Khatib ADA TADEA.
Sambamba na hilo Rais alitangaza majina ya manaibu mawaziri saba ambao ni Harusi Said Suleman Naibu Waziri katika Wizara ya Afya ambapo naibu wa wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali ni mmanga Mjengwa Mjawiri.
Naibu waziri wa Ujenzi Mawasiliano Ujenzi mawasiliano na u safirishajini Muhammed Ahmed Salum na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Naibu wake atakuwa Lulu Msham Khamis.
Katika Wizara ya habari,Utalii, utamaduni na Michezo Naibu wake atakuwa Bi Chumu Kombo Khamis na wizara ya Ardhi,Maji, Nishati na Mazingira Naibu wake atakuwa Juma makungu Juma na Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma, Utawala bora ni Juma Khamis Maalim
Alisema Mawaziri wote pamoja manaibu wao hao anategemea kuwalisha viapo vya utii kesho saa nne hapo Ikulu Mnazi MMoja Zanzibar.
Alisema wote aliowataja lazima wawajibike na kama aliyekuwa hawezi basi asema apumzike lakini kinachotakiwa ni kuona utendaji wa hali ya ujuu.
“Kama mtu hataweza kazi sitomvumilia hata siku moja ataondoka tuu” alisema Shein.
Alisema katika Safu yake hiyo atahakikisha kuwa wanafanyakazi za wananchi ipasavyo ili kero zao ziweze kutatuliwa.
No comments:
Post a Comment