NA MWANDISHI WETU
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameitaka kampuni maarufu
ya matairi nchini ya Superdoll kuendeleza uwekezaji katika maeneo ya ukanda wa
kilimo kwa ajili ya kuinua sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya nchi na watu
wake.
Mama Samia aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika hafla ya
uzinduzi wa kituo cha huduma za magari cha kisasa cha Superdoll na matairi ya
BF Goodrich KO2, jijini Arusha ambayo yatakuwa ufumbuzi wa tatizo sugu la
matairi yasiyo na kiwango hivyo kushindwa kuhimili mazingira ya barabara za
mbugani.
Kupitia hafla hiyo ya uzinduzi iliyoshuhudiwa pia na Mkuu wa
Mkoa wa Arusha, Daud Felix Ntibenda, Mama Samia alimpongeza Mkurugenzi wa
kampuni ya Superdoll, Seif A. Seif kwa kumwalika katika hafla hiyo iliyompa
fursa ya kusalimiana na wadau wa sekta binafsi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni hiyo (Seif), mbali ya
kumshukuru Mama Samia kukubali ombi la kumtaka awe mgeni rasmi katika uzinduzi
wa matairi bora ya BF Goodrich K02, alisema matairi hayo yatasaidia sekta ya
utalii kwa mkoa wa Arusha.
Alisema Seperdoll ambayo ni wasambazaji wa matairi namba
moja kwa ubora duniani ya Michelin, ni fahari kwao kuwekeza katika ujenzi wa
kituo cha kisasa cha BF Goodrich kwa kuwa na mashine zenye ubora wa hali ya
juu.
“Uwekezaji huu umelenga zaidi kwenye kuhakikisha tunakuza
wiwango vya usalama barabarani kwa wananchi na kwa watalii wanaokuja nchini.
Kwa njia hii tutaweza kukuza kukuza zaidi soko letu la
sekta ya utalii na kuongeza pato la taifa,” alisema Seif.
Seif alitoa wito kwa wadau mbalimbali wa sekta ya utalii wa
jijini Arusha kukitumia kituo hicho kikamilifu huku akiahidi kuwa huduma
itakuwa bora chini ya mawakala wao waliopo jijini Arusha
na Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment