Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi, John Kijazi (katikati) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondon, Ally Hapi (kulia) alipotembelea katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo.
Wagonjwa wakiwa wamelala wanne katika kitanda kimoja wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi, John Kijazi katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi, John Kijazi (katikati) akiwa katika wodi ya watoto Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi, John Kijazi akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika wodi ya watoto hospitali ya Mwananyamala.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi, John Kijazi (wa pili kushoto), akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondon, Ally Hapi (wa tatu kushoto) alipotembelea katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi, John Kijazi (wa pilikulia) akipokea msaada wa magodoro 50 kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Makanisa ya Kipentekoste Tanzania Askofu Saldonic Simon Sinde.
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI
imesema itaanza kutumia mbinu mpya kuwadhibiti madaktari na wauguzi wanaoiba
dawa za serikali na kisha kuziuza kwenye maduka ya watu binafsi.
Tamko hilo
lilitolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi alipoenda kukabidhi
magodoro 50 katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dar es Salaam Mwananyala yaliyotolewa na umoja wa makanisa ya Kipentekoste
nchini.
Kijazi
alisema mbinu hiyo itasaidia kuwabaini kiurahisi watumishi hao kwani
itaendeshwa kwa siri ambapo kila kitengo katika wizara ya afya kutakuwa na
mwakilishi atakayesaidia kutoa taarifa pindi atakapoona jambo hilo.
“Mimi
niwatake wenye tamaa waache mara moja haiwezekani dawa serikali inunue kwaajili
ya kuwapatia wananchi bure mtu mmoja kwa manufaa yake azipeleke kwa
wafanyabiasha kuuza wananchi wakose dawa na kuanza kuhangaika”alisema Kijazi.
Pia
amewataka wauguzi kuhakikisha kwamba malalamiko yanayotolewa na wananchi
yanafanyiwa kazi mara moja na kuongeza serikali hatitasita kumchukulia hatua
mtu yeyote atakayebainika kumnyanyasa mgonjwa.
Alisema
wagonjwa wamekuwa wakitoa malalamiko mengi juu ya huduma zinazotolewa katika
hospitali ya Mwananyamala hivyo amewataka watendaji kubadilika ili kuepuka
malalamiko yasiyo ya msingi.
Alisema ni
lazima watoa huduma za afya wakazingatia nidhamu na weledi katika utendaji wa
kazi kwani hawakulazimishwa kusomea taaluma hiyo na kuongeza kuwa fani zipo
nyingi hivyo ambaye anaona hawezi kufanya yanayotakiwa aachie wengine.
Pamoja na
hayo amezitaka hospitali zote kuanzisha dawati la malalamiko ili wanaohudumiwa
wapate pakusemea pindi wanapofanyiwa vitendo vya unyanyasaji ikiwa ni pamoja na
kucheleweshewa huduma au kuombwa fedha
ili kuwahishiwa huduma ili hali ikiwa ni haki yao.
Hata hivyo
ametaka madawati hayo kuwa wazi masaa 24 ili wananchi wapate mda mwingi wakujieleza na
sio kusubiri kuelezea hisia zao pale wanapoona viongozi wakitembelea vituo
hivyo.
Kijazi
alitembelea hodi mbalimbali hospitalini hapo ikiwamo wodi ya wazazi, Wanaume,
Watoto, Wanawake na watoto njiti ambapo alipata kujionea baadhi ya wagonjwa
wakilala zaidi ya mmoja kwenye kitanda kimoja kutokana na kukosekana kwa
vitanda.
Naye Mganga
mkuu msaidizi katika hospitali hiyo Delila Moshi alieleza matatizo
yanayoikabili hospitali hiyo kuwa ni pamoja na madeni ambapo inadaiwa stahiki
za watumishi Sh. milioni 500 ambazo ni fedha za likizo kwa wafanyakazi, Sare za kazi, Nyumba na posho za
masaa ya ziada.
Moshi
alisema hospitali hiyo pia ina ukosefu wa vifaa vya kisasa kama CT Scan hali
inayosababisha wagonjwa kupewa rufaa ya kwenda muhimbili kwaajili ya vipimo
zaidi, Ukosefu wa chumba cha uangalizi wa wagonjwa mahututi (ICU) na Daktari
bingwa wa mifupa na wagonjwa wa dharura.
Tatizo
lingine ni wingi wa wagonjwa wa msamaha ambapo kwa kuanzia januari hadi desemba
mwaka jana zaidi ya bilioni 2 zilitumika huku kwa mwezi wakitoa matibabu ya
zaidi ya milioni 100 bure.
No comments:
Post a Comment