BANKI ya 'AccessBank' inayoshiriki Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam imeendelea kutambulisha akaunti yake ya 'RAHISI' yenye mvuto mkubwa kwa wajasiliamali mbalimbali.
Akizungumza leo kwenye Banda la AccessBank kwenye maonesho ya Sabasaba, Ofisa Masoko wa banki hiyo, Sijaona Simon alisema Rahisi akaunti ni miongoni mwa bidhaa zinazowavutia wajasiliamali wengi kutokana na muundo rahisi wa uendeshaji wa akaunti hiyo kwa wajasiliamali wa kawaida.
Alisema akaunti hiyo inafunguliwa papo hapo tena bila gharama zozote kwa mteja mjasiliamali anayeitaji na hakuna gharama za uendeshaji huku ikiunganishwa na huduma za kibenki kwa kutumia simu ya mkononi ya mteja (AccessMobile).
Alisema faida zingine za akaunti hiyo ni kwamba mteja anaweza kuweka na kununua muda wa maongezi bila makato na hata kuhamisha fedha zake.
"Akaunti ya Rahisi ni nzuri sana kwa Wajasiliamali wote maana inafaida lukuki waje katika banda letu lililopo ndani ya Sabasaba Hall namba 9 na 10 mkabala na Banda la Bodi ya Kahawa...kuna mambo mengi na mazuri tumewaletea Watanzania hivyo waje kushughudia," alisema Simon.


No comments:
Post a Comment