Meneja wa Benki ya CRDB tawi
la Kasulu mkoani Kigoma Paul Chacha
akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi Mkuu wa Wilaya Kakonko madawati 100 yenye thamani ya Sh. Mil 5 yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa
madawati katika Shule za Msingi wilayani humo.
Mkuu wa wilaya Kakonko mkoani Kigoma
Kanali Hosea Ndagala akizungumza kabla hajapokea
madawati 100 yaliyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Shule za Msingi wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagaa (kulia) akipokea sehemu ya msaada wa madawati 100 kutoka kwa Meneja wa CRDB Tawi la Kasuu, Paul Chacha. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Hamashauri ya Wilaya ya Kakonko, Lusubilo Mwakibibi (katikati) na ofisa wa CRDB.
Mkuu
wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala (walioka kulia) akiwa
na Meneja wa CRDB Tawi la Kasulu, Paul Chacha (katikati) na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Kakonko, Lusubilo Mwakibibi. Kushoto waliosimama ni Katibu
Tawala wa Kakonko, Zainab Mbunda.
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, Kanali Hosea
Ndagala (kulia) akimshukuru Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Kasulu, Paul Chacha
baada ya kupokea msaada wa madawati 100 kwa ajili ya Shule za Msingi Wilayani
humo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Lusubilo Mwakibibi.
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala (katikati) akiwa na Meneja wa CRDB Tawi la Kasulu, Paul Chacha (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kakonko, Lusubilo Mwakibibi (kushoto) na Katibu Tawala wa Kakonko, Zainab Mbunda.





No comments:
Post a Comment