HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 08, 2016

JERRY MURO AFUNGIWA MWAKA MMOJA JELA YA SOKA

Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Wilson Ogunde akisoma maamuzi ya kamati hiyo iliyoketi jijini Dar es Salaam kuhusu shauri la msemaji wa Yanga, Jerry Muro ambapo kamati hiyo imetoa hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja kutojihusisha na masuala ya soka. (Picha na Francis Dande)

KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF, chini ya Mwenyekiti wake Wakili Wilson Ogunde imemfundia Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga Jerry Muro kujiusisha na masuala ya soka kwa muda wa mwaka mmoja sambamba na faini y ash mil 3 kutokana na maneno yake ya uchochezi.

Awali kamati hiyo iliyokutana Julai 2 mwaka huu, ilishindwa kutoa uamuzi dhidi ya Muro kutokana na madai ya kukosa wito uliomuelekeza rasm kuitwa na Kamati hiyo, huku kamati hiyo ikitaka Sekretariet ya TFF kumuita tena katika kikao cha  kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kutoa hukumu hiyo  Ogunda amesema, baada ya kupitia mashauri matatu yaliyowasilishwa juu ya kamati yake, kamati iliyapitia na kutoa hukumu kwa kusikiliza upande mmoja wa mshitaki kutokana na mshitakiwa kushindwa kufika katika kikao hicho.

Ogunda ametaja mashtaka hayo matatu yaliyofika mbele ya kamati yake kuwa ni kushindwa kutekeleza maamuzi ya kamati ya nidhamu iliyomtaka kulipa faini y ash mil 5 baada ya kupatikana na hatia Mei 5 mwaka jana, hivyo kutokana na kushindwa kutekeleza agizo hilo la kamati husika licha ya Mei 10 kukumbushwa na TFF kamati imejilidhisha na kumtia hatiani kwa kumfungia mwaka mmojakuanzia Julai 7 mwaka huu.

Aidha Ogunda aliyeambatana na Wajumbe wake watatu wa kamati hiyo akiwemo Makam wake Mwenyekiti Ebeneza Mshana alisema shitaka la pili lillilomtia hatiani Muro ni kutoa lugha ya kashfa kwa kupotosha  maamuzi ya TFF Juni 25 mwaka huu alitoa taarifa katika moja ya redia akipinga maamuzi TFF kusaini mkataba wa Azam TV kwa niaba ya CAF akidai TFF wanawahujumu ili wasipate mapato katika mchezo wao na Tp Mazembe. Kamati ya Maadili kamati imejiridhisha kuwa Muro hana hatia katika shitaka hilo la pili,,alisema.

Kuhusu Shitaka la tatu Ogunde alisema mnamo Juni 26 kupitia moja ya redia Muro alikaliliwa akivunja ukaaji wa mashabiki Uwanjani akidai wa Simba wanatakiwa kukaa juu ya paa kitendo ambacho kingepelekea vurugu wakati TFF walikuwa washatoa muongozo juu ya kukaa Uwanjani hapo.

Ambalo limemkuta na hatia ya kufungiwa mwaka mmoja ambayo adhabu yake inaanza Julai 7 mwaka huu na adhabu zote za kufungiwa zitaenda sambamba kwa maana ya kutumikia adhabu mbili kwa kipindi kimoja

Wakati huo huo kuhusu Nasseb Mabrouk ametakiwa kuhakikisha anarejesha kiasi cha sh 949,767 ndani ya siku 30 kwa TFF ambazo alishindwa kuziwasilisha akiwa msimamizi wa kituo cha Soka Mwanza.

No comments:

Post a Comment

Pages